Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lamine Yamal ampa mchecheto Kocha Argentina

Muktasari:

  • Katika Fainali za Kombe la Dunia ambazo zinafikia tamati kesho, Yamal amehusika na mabao mawili tu ya Hispania kwenye mashindano hayo akifunga bao moja na kupiga pasi moja ya mwisho.

Kocha Mkuu wa Argentina, Lionel Scaloni amemtaja winga wa Hispania, Lamine Yamal kama mchezaji tishio zaidi kwao katika mechi ya Fainali ya Kombe la Dunia itakayochezwa kesho Jumapili, Julai 19, 2026 kuanzia saa 4:00 usiku kwa muda wa Afrika Mashariki katika Uwanja wa MetLife, New Jersey, Marekani.

Lamine Yamal hakuanza vizuri mashindano hayo kwa vile alikuwa ametoka kupona majeraha lakini katika mechi za mwishoni ameonekana kuanza kuonyesha makali yake na ndiye aliifanya Hispania kupata mkwaju wa penalti uliozaa bao la kwanza katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ufaransa katika nusu fainali, baada ya kuchezewa rafu katika eneo la hatari na Lucas Dinge.

Lakini Scaloni anaamini kwamba licha ya kutokuwa na takwimu nzuri katika mashindano hayo, Lamine Yamal anabakia kuwa mchezaji tishio zaidi wa Hispania na anatamani hata mchezaji huyo asicheze dhidi yao kwenye fainali.

"Lamine (Yamal) ni mchezaji wa kipekee sana. Kijana huyu ni hazina kwa mchezo wa soka na bado ni mdogo sana, akiwa na mengi zaidi ya kuonyesha. Natamani tungemfungia chumbani kesho.️

"Ni kipaji ambacho kitailetea Hispania furaha kubwa sana siku zijazo lakini tunatumaini hilo halitatokea Jumapili.

"Yeye, kama Leo (Messi), ni mmoja wa wale wachezaji ambao ni vigumu sana kuwadhibiti uwanjani," amesema Scaloni.

Katika Fainali za Kombe la Dunia ambazo zinafikia tamati kesho, Yamal amehusika na mabao mawili tu ya Hispania kwenye mashindano hayo akifunga bao moja na kupiga pasi moja ya mwisho.

Bao moja alifunga katika mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Saudi Arabia ambao Hispania iliibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Pasi pekee ya mwisho ambayo Yamal amepiga ni katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Ufaransa.