Levy afuta usajili Spurs, aelekeza nguvu ukarabati wa uwanja

Muktasari:

  •  Spurs ndiyo timu pekee kwenye Ligi Kuu England ambayo haijafanya usajili kwenye dirisha hili la usajili na ripoti zikidai kwamba pesa za timu hiyo zinatumika zaidi kwenye kujenga uwanja mpya, hivyo wanaweka bajeti yao sawa.

Mwenyekiti wa Tottenham Hotspur, Daniel Levy amesisitiza kwamba hatafanya usajili wowote katika dirisha hili labda kama tu atakuwa ameshawishika kwamba mchezaji huyo atakayemsajili atakuwa kuleta kitu kipya kwenye kikosi chao.

 Spurs ndiyo timu pekee kwenye Ligi Kuu England ambayo haijafanya usajili kwenye dirisha hili la usajili na ripoti zikidai kwamba pesa za timu hiyo zinatumika zaidi kwenye kujenga uwanja mpya, hivyo wanaweka bajeti yao sawa.