Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majeruhi wamtesa Arteta Arsenal

Nahodha wa Arsenal, Martin Odegaard ambaye alishindwa kuendelea na mechi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid, Aprili 29, 2026. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Hali imezidi kuwa tete baada ya nahodha Odegaard kuonekana kupata maumivu katika mchezo dhidi ya Atletico Madrid huku Arteta akisema wanasubiri tathimini ya madaktari kujua hali yake.

London, England. Wakati takwimu zikionesha wachezaji wa Arsenal wamekosa jumla ya mechi 262 kwa klabu na timu za taifa msimu huu huku 141 kati ya hizo zikiwa ni ndani ya Ligi Kuu pekee, kocha wa kikosi hicho, Mikel Arteta ameamua kuchukua uamuzi wa haraka kutatua tatizo hilo.

Uamuzi wa Arteta umekuja kufuatia kuelekea mwisho wa msimu huku akilenga kumaliza na mataji mawili yaliyobaki, Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hali ikiwa hivyo Arsenal, wapinzani wake wakubwa katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City, wachezaji wake wamekosa mechi 135 pekee kutokana na majeraha, lakini kinachoumiza zaidi Arsenal ni kukosekana kwa mshambuliaji wao muhimu Kai Havertz ambaye amecheza mechi chache sana huku nyota wa Man City, Erling Haaland akikosa mchezo mmoja wa ligi.

Arteta ameonekana kuchoshwa na wimbi la majeruhi linaloikumba timu hiyo, hali iliyomlazimu kuchukua hatua nzito na kuamua kumpa kazi maalum mtaalamu kuchunguza tatizo hilo linalotishia kuvuruga mwenendo wao msimu huu.

Arsenal ambayo hadi jana Jumamosi ilikuwa ikiongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi 73 kabla ya kucheza na Fulham, bado ipo kwenye mbio za kuwania makombe mawili, huku ikikumbwa na pigo la kukosa nyota wake muhimu hali iliyowafanya ionekane kuwa butu hasa safu ya ushambuliaji.

Mastaa kama Martin Odegaard, Bukayo Saka na Kai Havertz wamekosa sehemu kubwa ya msimu kutokana na majeraha.

Katika jitihada za kutafuta suluhisho, Arteta amemvuta rafiki yake wa karibu, mtaalamu wa tiba ya viungo kutoka Hispania, Joaquín Acedo, kusaidia kuchunguza chanzo cha tatizo hilo.

Acedo ana uhusiano wa karibu na Arteta na amewahi kufanya kazi na timu hiyo hapo awali huku akionekana mara kadhaa katika kituo cha mazoezi cha London Colney.

Licha ya kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi tatu, Arsenal wako kwenye presha kubwa kwani Pep Guardiola na Manchester City wana mchezo mkononi hali inayoweza kubadili kabisa msimamo.

Mashabiki wa Arsenal wana hamu kubwa ya kumaliza ukame wa zaidi ya miaka 20 bila ubingwa wa ligi lakini wimbi la majeruhi linaendelea kuwa tishio kubwa.

Hali imezidi kuwa tete baada ya nahodha Odegaard kuonekana kupata maumivu katika mchezo dhidi ya Atletico Madrid huku Arteta akisema wanasubiri tathimini ya madaktari kujua hali yake.

Akizungumza kabla ya kuivaa Fulham, Arteta alikiri ukubwa wa tatizo hilo akisema: “Kai amekuwa pigo kubwa kwetu. Ni mmoja wa wachezaji muhimu sana katika safu ya ushambuliaji na amekosekana kwa muda mrefu.”