Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City hali tete

Manchester, England. Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amekiri wanapitia wakati mgumu baada ya kucheza mechi nne za mwisho za Ligi Kuu England bila ya kupata ushindi.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu msimu uliopita, walibeba pia Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Msimu huu wameshindwa kupata ushindi dhidi ya Chelsea, Liverpool, Tottenham na Aston Villa.

Kipigo cha 1-0 dhidi ya Aston Villa uwanjani Villa Park walichokipata Jumatano usiku kimewavuruga wachezaji wa Man City akiwemo straika wa mabao, Erling Haaland, huku wakishuka hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Guardiola aliweka wazi baada ya kuchezea kichapo na Aston Villa; “Timu bora imeshinda, niliwaambia wachezaji wangu kwenye soka huwa inatokea, najua tulitaka kushinda, walijaribu lakini imeshindikana, matokeo si mazuri kama ilivyokuwa mechi za nyuma.

“Lazima niangalie hili kwa kina ili kupata ufumbuzi, nitarudia mechi kuona makosa yetu, nina jukumu la kubadilisha timu irudi katika hali yake, kuna wakati unaweza kucheza vizuri, pia kuna wakati unakosea. Lazima tubadilike.”

Man City ilipiga mashuti mawili tu dhidi ya Villa ambayo ni mashuti machache zaidi kupigwa chini ya Guardiola anayesifika kwa soka safi, huku mwenyeji akipiga mashuti 22.

Juhudi za Leon Bailey ziliwapa faida Villa huku Man City ikitafakari kwani ilipania kuendeleza rekodi msimu huu, hata hivyo mambo yamekuwa tofauti.

Man City inapitia kipindi  kigumu ikiwa wiki chache tu baada ya kukubali tarehe ya kusikiliza kesi za tuhuma za kukiuka sheria za matumizi ya pesa Ligi Kuu England.

Kabla ya mechi dhidi ya Villa, Guardiola alisisitiza alipania kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England kwa mara ya nne mfululizo, hata hivyo wakakutana na kichapo.

“Sipendi kuzungumzia maoni ya wachambuzi, pengine sitakuwa sawa lakini sijali, najua wachambuzi walivyokuwa, tumeonyesha kitu cha tofauti sana, hii itatusaidia sana, naamini tutachukua tena msimu huu,” alisema Guardiola

Kauli ya Guardiola aliwajibu wachambuzi wa soka wa Sky Sports, Jamie Carragher na Roy Keane, ambao wanaipigia debe Arsenal kuwa itabeba ubingwa msimu huu.

Carragher alifunguka na kudai: “Ukituuliza nadhani kila mtu anatamani kuona Man City ikibeba ubingwa, tumeona msimu uliopita, Man City ilikuwa inashinda mechi zake mfululizo tofauti na timu nyingine, nadhani Arsenal imepambana sana msimu huu, ni vizuri kuona Man City ikipoteza pointi. Kwa vile msimu uliopita tulibeba makombe matatu? Unadhani hakuna timu ya kumzuia? Hapana.”

Kwa upande wa Keane alisema: “Nisingeweka dau dhidi ya Man City, lakini nimeanza kuwa na mashaka na kiwango chao msimu huu, haionyeshi kama ina njaa ya mafanikio kama ilivyokuwa msimu uliopita.”