Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City ilivyokatwa upepo mbio za ubingwa EPL

Muktasari:

  • Licha ya kuonyesha uimara kwa kurejea mchezoni, matokeo hayo bado ni pigo kwa City ambao walihitaji ushindi ili kuendelea kuwa kwenye nafasi nzuri ya ubingwa.

Liverpool, England. Manchester City wamejikuta wakibaki midomo wazi kwa kile kilichotokea usiku wa jana katika mwendelezo wa mechi za Ligi Kuu England ambayo inaelekea ukingoni.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Hill Dickinson, wenyeji Everton waliondoka kipindi cha kwanza wakiwa nyuma kwa bao moja ambalo liliwekwa kambani dakika ya 43 na Jérémy Doku.

Hata hivyo, kipindi cha pili kulianza tofauti kabisa na ilivyotarajiwa baada ya vijana wa kocha David Moyes kurejea mchezoni dakika ya 68 kwa bao la kusawazisha lililofungwa na Thierno Barry ambaye alitumia vyema makosa ya beki Marc Guehi.

Mshambuliaji wa Everton, Thierno Barry wakati akifunga bao katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Man City. Picha na Mtandao

Zilipita dakika tano Everton wakapata bao lingine, wakati huu akifunga Jake O'Brien kabla ya Barry kurudi tena kambani kufunga bao la tatu dakika ya 81.

Erling Haaland alirejesha matumaini kwa City baada ya kufunga bao la pili dakika ya 83 aliposetiwa pasi na kiungo mkongwe Mateo Kovačić. Hata hivyo, Everton waliendelea kuzuia mashambulizi ya wababe hao lakini Doku alifunga bao la kusawazisha dakika za majeruhi na kuondoa matumaini ya ushindi kwa Everton.

Licha ya kuonyesha uimara kwa kurejea mchezoni, matokeo hayo bado ni pigo kwa City ambao walihitaji ushindi ili kuendelea kuwa kwenye nafasi nzuri ya ubingwa.

Baada ya kupoteza pointi mbili Man City wataendelea kusalia nyuma ya wapinzani wao Arsenal wanaoongoza ligi hiyo kwa tofauti ya pointi nne huku wakihitaji ushindi katika michezo yao mitatu iliyosalia ili kutwaa taji hilo.

Nyota wa Man City, Earling Haaland (kushoto), mwingine kulia ni Rayan Cherki wakati wakionekana kusikitika na matokeo ya sare waliyopata dhidi ya Everton. Picha na Mtandao


Maoni ya wachambuzi

Mchambuzi wa soka Jamie Carragher ametoa utabiri wake kuhusu mbio za ubingwa wa EPL kufuatia sare hiyo ya mabao 3-3 kati ya Manchester City na Everton.

Carragher anaamini kuwa ubingwa unaweza kuamuliwa katika mchezo ujao wa Arsenal dhidi ya West Ham United, akidai ushindi katika mechi hiyo unaweza kuwahakikishia taji hilo.

Kwa upande wake, mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry ametoa tahadhari, akisisitiza kuwa bado hakuna kilichomalizika na timu hiyo inapaswa kuwa makini hadi mwisho wa msimu.

Henry amebainisha kuwa presha imehamia kwa Arsenal, huku City wakionekana kupoteza mwelekeo baada ya kufanya makosa yaliyoiruhusu Everton kurejea mchezoni.