Manara: Nililala kwenye kochi

Wednesday August 04 2021
By Mwandishi Wetu

ALIYEKUWA msemaji wa Simba Haji Manara amedai kuwa ilimlazimu kulala kwenye kochi wakati kikosi cha timu hiyo kiliposafiri nchini Afrika Kusini kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Manara alidai sababu kubwa ya kulala kwenye kochi ni kutokana na kutopewa kipaumbele na mabosi wa timu hiyo.

"Nimefanya kazi ya kujitolea kwenye hii klabu mpaka kufikia hatua ya kusafiri kwa gharama zangu mwenyewe bila hata kupewa na uongozi, hii ni kuonyesha kabisa ni jinsi gani uongozi wa sasa umekuwa ukinifanyia vitu vya kinyama na nisivyotarajia" alisema.

Katika hatua nyingine Manara alidai kuwa hata safari za nje ya nchi pindi Simba inaposafiri amekuwa akitumia fedha zake binafsi kwa sababu ya kutowekwa kwenye orodha ya viongozi wanaosafiri na timu.

"Licha ya hamasa kubwa ambayo naifanya lakini cha ajabu nilikuwa nikijilipia mwenyewe kuanzia usafiri, malazi N.K na nilipokuwa niukiuliza naambiwa sikuwa kwenye mipango ya kusafiri na timu lakini sikukata tamaa bali niliendelea kuipigania klabu hii kwa nguvu kubwa" alidai Manara.

IMEANDIKA NA DAUDI ELIBAHATI

Advertisement
Advertisement