Manji awatuliza wanayanga

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji

Muktasari:

Jana, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilitoa zuio la mkutano huo uliopangwa kufanyika kesho (Jumapili) baada ya shauri lililowasilishwa na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo.

Dar es salaam. Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji amewataka wanayanga kutulia na kuheshimu zuio la kutofanya mkutano wao mkuu wa dharura.

Jana, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilitoa zuio la mkutano huo uliopangwa kufanyika kesho (Jumapili) baada ya shauri lililowasilishwa na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo.

Akizungumza leo (Jumamosi) katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mtaa wa Jangwani jijini hapa, Manji aliwataka wanachama kutulia na kuheshimu zuio hilo ili kuwapa fursa viongozi kulishughulikia.

"Nawaomba wanayanga waheshimu zuio la mahakama, na kesho hakutakuwa na mkutano kama tulivyopanga.Viongozi tutahakikisha tunalipatia ufumbuzi jambo hilo ili tufanye mkutano wetu mbeleni,"Manji.