Masau Bwire: Morrison hatari sana

Monday June 07 2021
morrison pic
By Olipa Assa

WINGA machachali wa Simba Bernard Morrison ametajwa kuwa mchezaji wa kuchungwa zaidi ndani ya dakika 90 kutokana na namna ambavyo anapambana kupata matokeo.

Morrison alitua Simba akitokea kwa watani zao Yanga licha ya kudaiwa kuwepo kwa kesi katika mahakama ya usuluhisi (CAS)lakini ameonekana kuwa na msaada mkubwa anapopata nafasi ya kucheza.

Katika mchezo wa mwisho ambao Simba walicheza dhidi ya Ruvu Shooting Morrison ni miongoni mwa wafungaji katika ushindi wa ambao 3-0 ambayo yalifungwa huku bao lake likiwa gumzo baada ya kufumua shuti nje ya 18.

Masau Bwirwe Mkuu wa Idara ya Habari ya Ruvu Shooting anasema, uwezo wa Morrison na ujanja wake unatakiwa kutizamwa kwa kina na waamuzi ambao wanasimamia michezo husika.

Amesema katika mchezo wao uliopita hakustaili kupewa penati kwa madai alijiangusha na kumdanganya mwamuzi hivyo wanatakiwa kumwangali kwa jicho la tatu.

"Huyu Morrison ni mjanja mjanja sana hivyo waamuzi wamuangalie sana huyu mtoto anajirusha sana," amesema Bwire.

Advertisement


Advertisement