Mashabiki wehu wa soka Nigeria sasa wageukia timu ya kikapu Olimpiki

Muktasari:

Kwa muda mrefu mpira wa miguu umekuwa mchezo kipenzi kwa Wanigeria baada ya mafanikio ya kihistoria ya kutwaa medali ya dhahabu katika Olimpiki, lakini sasa nchi hiyo imeelekeza macho kusubiria mafanikio katika mpira wa kikapu jijini Tokyo.

Abuja, Nigeria (AFP)
Kwa muda mrefu mpira wa miguu umekuwa mchezo kipenzi kwa Wanigeria baada ya mafanikio ya kihistoria ya kutwaa medali ya dhahabu katika Olimpiki, lakini sasa nchi hiyo imeelekeza macho kusubiria mafanikio katika mpira wa kikapu jijini Tokyo.
Taifa hilo la Afrika Magharibi lenye watu milioni 210, liliweka historia miaka 25 iliyopita wakati timu yake ya soka ilipotwaa medali ya dhahabu katika Michezo ya Olimpiki jijini Atlanta kwa kuishinda Argentina, hiyo ikiwa medali ya kwanza kwa timu ya Afrika.
Lakini kwa michezo inayoendelea Tokyo, timu zote za soka za wanawake na wanaume zimeshindwa kufuzu, hivyo matumaini ya medali yakihamia kwenye michezo mingine, ikiwemo timu ya mpira wa kikapu ya wanaume, D'Tigers', baada ya kupata matokeo ya kushtua wakati wa kipindi cha kuelekea Olimpiki.
Ikishika nafasi ya 22 kw aubora duniani, Nigeria iliishangaza Marekani, ambayo ina wachezaji nyota wa NBA kama Kevin Durant, kw akuishinda kwa pointi 90-87, ikiwa imecharazwa kwa pointi 156-73 na wapinzani wao kwenye michezo iliyofanyika jijini London mwaka 2012.
Wanigeria hao pia waliwastua Waargentina, ambao wanashika nafasi ya nne kwa ubora duniani, kwa kuwalaza kwa pointi 94-71 katika mechi nyingine ya kujipima nguvu kwa ajili ya michezo ya Tokyo.
"Bado hatujashinda, lakini nina hisia kuwa tunaweza kulibeba bara zima," alisema kocha Mike Brown, 51, ambaye aliwahi kuzifundisha Los Angeles Lakers na Cleveland Cavaliers.
"Hatuenda kutafuta uzoefu, tunakwenda Tokyo kushinda," he said.
"Ushindi huu unaoongeza morali kabla ya michezo iliyoahirishwa ya Olimpiki ya Tokyo ni ishara nzuri kwamba Team Nigeria itamaliza katika nafasi ya kutwaa medali," aliongeza Waziri wa Michezo wa Nigeria, Sunday Dare.                       
Kama ilivyo timu ya taifa ya soka ya Nigeria, kikosi cha 'D'Tigers' kimetawaliwa na wanaochezo Ligi ya Taifa ya Kikapu Marekani (NBA).
Wana nguvu katika kika eneo, huku wachezaji watatu wa klabu ya Miami Heat-- Gabe Vincent, Precious Achiuwa na KZ Okpala-- wakiwa sehemu ya timu hiyo, sambamba na mlinzi wa Minnesota Timberwolves, Josh Okogie na mchezaji wa kati wa Detroit Pistons, Jahlil Okafor.