Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maskini! Mchezaji afia uwanjani Gabon

Muktasari:

  • Katika Ligi Kuu Gabon huyu anakuwa mchezaji wa saba amefariki katika kipindi cha miaka 12 iliyopita.

Libreville, Gabon. Mchezaji Herman Tsinga amefariki dunia muda mfupi baada ya kuongana kichwa akiwa mpira na mwenzake.

Tsinga ni mchezaji wa Akanda FC inayoshiriki Ligi Kuu Gabon alipatwa na mkasa huo baada ya kudondoka katika ya uwanja.

Gari la wagonjwa liliwahi kuingia kiwanjani na kumsaidia kumpa huduma ya kwanza kabla ya kumchukua katika machela.

Lakini pamoja na juhudi za madaktari hao kumkimbiza hospitali Owendo, baadaye ilitangazwa kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 30, amefariki.

Tukio hilo la lisikitisha lilitokea katika dakika 23 ya mchezo kati ya Akanda dhidi ya Missile FC.

Haiko wazi ni muda gani hasa Tsinga alifariki, lakini Africa News imeripoti kuwa “alipewa matibabu ya kushtua moyo katika hospitali ya jeshi".

Gazeti la The Union la Gabon liliripoti kuwa, hata gari la wagonjwa lililoingia uwanjani halikuwa vifaa hata mtungi wa gesi wa kumsaidia kupumua haukuwemo katika gari hiyo.

Huyu ni mchezaji wa saba amefariki katika miaka 12 iliyopita katika Ligi Kuu Gabon.