Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe, Dembele walivyoipeleka Ufaransa nusu fainali

Muktasari:

  • Ufaransa ikalazimika kusubiri mpaka dakika 45 za pili kupata mabao hayo,  baada ya Morocco kuikomalia kipindi cha kwanza kikimalizika kwa timu hizo bila bao.

Ufaransa imeendelea kuwa mwiba kwa Morocco, ikifanikiwa kurudia ushindi wa mabao 2-0 na kuihakikishia nafasi ya kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Dunia 2026.

Ufaransa ikalazimika kusubiri mpaka dakika 45 za pili kupata mabao hayo,  baada ya Morocco kuikomalia kipindi cha kwanza kikimalizika kwa timu hizo bila bao.

Mshambuliaji na nahodha wa Ufaransa, Kylian Mbappe, alikosa mkwaju wa penalti dakika ya 27 uliodakwa vizuri na kipa Yassine Bounou.

Ufaransa licha ya kutawala mchezo ikitengeneza nafasi 13  lakini ni mashuti matatu pekee yaliyolenga lango huku Bonou akiwa shujaa kwenye kipindi hicho cha kwanza akiokoa nafasi tatu.

Morocco haikuwa na nguvu kubwa kwenye mashambulizi yake, ikimaliza kipindi cha kwanza bila kuwa na shuti lililolenga lango.

Alikuwa Mbappe akisawazisha makosa yake akiifungia Ufaransa bao la kwanza dakika ya 59 kwa shuti zuri la kiufundi akipokea pasi ya winga Michael Olise.

Bao hilo linakuwa la nane kwa Mbappe kwenye fainali za mwaka huu akiendelea kumkaba koo nahodha wa Argentina, Lionel Messi wote wakifunga idadi sawa.

Mbappe pia bao hilo linamfanya kufikia mabao nane ambayo aliyafunga kwenye fainali zilizopita zilizofanyika Qatar.

Ufaransa ikapata bao la pili dakika ya 65 likifungwa na Dembele kwa shuti kali lililomshinda nguvu Bounou na kujaa wavuni akipokea pasi ya Mbappe.

Morocco ikatengeneza nafasi nzuri dakika ya 83 kiungo Azzedine Ounahi shuti lake lililotokana na shambulizi la adhabu ndogo likapanguliwa na kipa Mike Maignan, likiwa ndio shuti la kwanza kwao lililolenga lango kwenye mchezo huo.

Mpaka mwisho wa mchezo Ufaransa ikafanikiwa kutoka na ushindi huo wa mabao 2-0, ikitinga nusu fainali ya tatu mfululizo katika michuano hiyo, ikirudia kipigo hicho ilichowapa Waarabu hao kwenye fainali zilizofanyika Qatar mwaka 2022.