Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi aaga kwa mabao akiiweka katika mabano Argentina

Muktasari:

Messi ndio Mfungaji Bora wa muda wote wa timu ya Taifa ya Argentina akiwa amepachika mabao 114 katika michezo 194 ya kimashindano.

Lionel Messi usiku wa kuamkia leo ameiongoza Argentina kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 nyumbani dhidi ya Venezuela lakini baada ya hapo akatoa kauli inayoonekana kama ni ya kuwaaga kwa mara ya mwisho mashabiki ndani ya ardhi ya kwao.

Messi ambaye katika mchezo huo alipachika mabao mawili huku lingine likifungwa na Lautaro Martinez amesema kuwa hafikirii kama atakuwa na muda mrefu wa kuitumikia timu ya taifa ya nchi hiyo.

Baada ya mchezo huo, Argentina haitocheza tena mechi ya kimashindano katika ardhi ya kwao hadi Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakapomalizika huko Marekani, Canada na Mexico jambo ambalo linamfanya Messi ajione kama analazimika kuwaaga mashabiki wa nyumbani.

"Kama nilivyosema hapo nyuma kuhusu Kombe la Dunia kwamba sidhani kama nitacheza tena. Kwa sababu ya umri wangu, kitu kinachoingia zaidi akilini ni sitoweza kucheza.


"Ninajitahidi kujisikia vizuri na zaidi ya yote kuwa mkweli kwangu. Pale ninapojisikia vizuri ninafurahi lakini nisipojisikia, sina muda mzuri hivyo nachagua kutokuwepo kule kama sitojisikia vizuri. Sijafanya uamuzi bado kuhusu Kombe la Dunia," amesema Messi.

Messi amesema kuwa bado anao muda wa kutosha kujitathmini na kufanya uamuzi kama ataitumikia Argentina katika Kombe la Dunia lijalo au hatofanya hivyo.

"Nitamaliza msimu kisha nitakuwa na maandalizi ya msimu na kutakuwa na miezi sita itakayobakia. Hivyo tutaangalia najisikiaje. Nitakuwa na maandalizi mazuri ya msimu mwaka 2026 na baada ya kumaliza msimu wa Ligi Kuu Marekani nitafanya uamuzi," amesema Messi.

Messi ambaye ni Mfungaji Bora wa muda wote wa Argentina na akiwa ndiye anaongoza kwa kucheza idadi kubwa ya mechi za timu ya Taifa ya nchi hiyo.

Argentina itacheza mechi ya mwisho ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Ecuador Jumatano Ijayo, Septemba 10, 2025 ambayo tayari Messi ameshasema kuwa hatocheza.

Akiwa na jezi ya timu ya Taifa ya Argentina, Messi ameshinda mataji yote makubwa ambayo timu hiyo imeshiriki huku yeye akiwa nahodha.

Argentina imeshinda Kombe la Dunia, Kombe la Copa America na Kombe la Finalissima huku Messi akitoa mchango mkubwa kikosini.