Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi atajwatajwa Ligi Kuu England

Muktasari:

  • Gwiji huyo wa soka amedaiwa kwamba anafikiria uhamisho wa mkopo kwenda kwenye ligi yenye ushindani mkali ili kujiweka sawa kwa ajili ya kungoza harakati za Argentina za kutetea ubingwa wa Kombe la Dunia mwakani.

MIAMI, MAREKANI: NDOTO za supastaa, Lionel Messi kucheza Kombe la Dunia 2026 akiwa kwenye viwango bora kabisa linaweza kumsukuma kwenda kucheza soka kwenye Ligi Kuu England akiwa na umri wa miaka 38.

Gwiji huyo wa soka amedaiwa kwamba anafikiria uhamisho wa mkopo kwenda kwenye ligi yenye ushindani mkali ili kujiweka sawa kwa ajili ya kungoza harakati za Argentina za kutetea ubingwa wa Kombe la Dunia mwakani.

Inter Miami inataka kumwongezea mkataba wa miaka miwili Messi, lakini hata kama atasaini dili jipya, mshindi huyo mara nane wa Ballon d’Or anaweza kuhamia kwa muda kwenye ligi kubwa za Ulaya.

Ripoti kutoka Argentina zinadai kwamba Messi anataka kwenda kucheza kwenye ligi yenye ushindani wa uhakika kabla ya kufika kwa fainali za Kombe la Dunia 2026 litakalofanyika Marekani.

Hiyo ina maana, mkali huyo wa zamani wa Barcelona anaweza kurudi kukipiga kwenye ligi za Ulaya kwa miezi kadhaa. Timu ya Messi, Inter Miami ilishiriki Kombe la Dunia la Klabu, lakini staa huyo aliduwazwa na timu yake na zamani, Paris Saint-German baada ya kuwasukuma nje kwa kipigo cha mabao 4-0 katika raundi ya 16 bora.

Bingwa huyo mara nne wa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Messi alidaiwa na mashabiki kwamba alitaka kumchapa ngumu mchezaji mwenzake wa zamani, Vitinha wakati wa mchezo huo.

Messi hajawahi kucheza Ligi Kuu England. Lakini, kocha wa zamani wa Manchester City, Mark Hughes alidai mmiliki wa timu hiyo, Sheikh Mansour alijaribu kumsajili wakati aliponunua klabu hiyo ya Etihad.

Na kocha wa sasa wa Man City, Pep Guardiola inafahamika pia alitamani kuungana na kijana wake huyo wa zamani wa Barcelona kabla ya kuhamia zake PSG mwaka 2021. Kuna uvumi pia, huenda Messi akarudi Barcelona.

Lakini, kwa mujibu wa mwandishi wa Hispania, Guillem Balague anaamini hilo halina uwezekano mkubwa wa kutokea kutokana na uhusiano mbaya uliopo baina yake na rais wa klabu hiyo, Joan Laporta.

Hivyo, Ligi Kuu England panaweza kuwa mahali pazuri kwa mkali huyo alifunga mabao 112 kwenye mechi 193 alizochezea timu ya taifa ya Argentina kwenda kukipiga.