Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mhesa alivyotibua Eid ya Yanga

Muktasari:

  • Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiww na pointi 38 ilizokusanya katika mechi 16.

Dar es Salaam. Yanga imefikisha idadi ya mechi 36 mfululizo za Ligi Kuu ya NBC ilizocheza bila kupoteza baada ya leo, Jumamosi, Machi 21, 2026 kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Mara ya mwisho kwa timu hiyo kupoteza mchezo wa Ligi Kuu ilikuwa ni msimu uliopita ilipofungwa mabao 3-1 na Tabora United (sasa TRA United), katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Novemba 7, 2024.

Katika mechi hizo 36 ambazo Yanga haijapoteza, michezo 30 imepata ushindi na sita imetoka sare.

Matokeo ya leo yameifanya Yanga iendelee kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha pointi 38 huku Mtibwa Sugar ikisogea hadi nafasi ya nane baada ya kufikisha pointi 22.

Yanga ndio ilitangulia kupata bao kupitia kwa Pacome Zouzoua katika dakika ya 23.

Pacome amefunga bao hilo akimalizia pasi iliyotokea upande wa kushoto ambayo imepigwa na Emmanuel Mwanengo.

Mwanengo alitumia vyema kosa la kipa Costantine Malimi aliyetema mpira wa shuti uliopigwa na Allan Okello na kumpasia Pacome aliyeujza wavuni.

Bao hilo lilidumu hadi katika dakika za majeruhi kabla ya Ismail Mhesa kutibua Eid ya Yanga alipofunga kwa mpira wa kona uliojaa moja kwa moja wavuni.

Matokeo ya leo yameifanya Yanga iendelee kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha pointi 38 huku Mtibwa Sugar ikisogea hadi nafasi ya nane baada ya kufikisha pointi 22.