Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Milan kumchomoa Hojlund Man United

Klabu ya AC Milan imewasilisha ofa ya mkopo wa msimu mzima wenye thamani ya pauni milioni 4 (Sh13 bilioni) kumchukua mshambuliaji wa Manchester United, Rasmus Hojlund, ambaye hana nafasi kwenye mipango ya kocha Ruben Amorim.

Hojlund, ambaye alisajiliwa na United mwaka 2023 akitokea Atalanta, aliachwa benchi bila kutumika kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Fiorentina, jambo lililoonyesha wazi kuwa Amorim hampangii majukumu msimu huu. Kabla ya pambano hilo, United ilimtambulisha rasmi mshambuliaji mpya Benjamin Sesko, aliyesajiliwa kwa pauni milioni 74 (Sh247 bilioni) kutoka RB Leipzig.

Taarifa zinaeleza kuwa United iko tayari kumuuza Hojlund kwa bei ya pauni milioni 30 pekee, lakini Milan wanataka mkopo wenye kipengele cha kumnunua kwa pauni milioni 39 endapo atafanya vizuri.

Licha ya hali hiyo, Hojlund mwenye umri wa miaka 22 amesisitiza nia ya kubaki na kupigania namba, akisema ushindani unamnoa na kuongeza ubora wa timu. Tangu ajiunge na United, amefunga mabao 26 katika michezo 95.

United ilihangaika majira haya ya joto kutafuta mshambuliaji namba tisa, ikiwemo kumuwinda Liam Delap aliyekwenda Chelsea, Viktor Gyokores (Arsenal) na Hugo Ekitike (Liverpool), kabla ya kumpata Sesko.

Sesko, ambaye alikataa ofa ya Newcastle, amesema mradi wa United umemvutia na anaamini ni mahali sahihi kufikia malengo yake, licha ya klabu hiyo kumaliza nafasi ya 15 kwenye Ligi Kuu msimu uliopita. Amorim pia ameongeza wachezaji wapya akiwemo Matheus Cunha na Bryan Mbeumo.

Wakati huo huo, United inaendelea kutafuta kiungo wa kati na imewasiliana na wawakilishi wa Carlos Baleba wa Brighton, ingawa Brighton hawana mpango wa kumuuza.