Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miloud Hamdi mambo magumu Misri, Ismaily hali tete

Muktasari:

  • Ismaily imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Misri mara tatu tofauti ambazo ni 1966–67, 1990–91 na 2001–02 na imewahi kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1963.

Miloud Hamdi alijiunga na Ismaily ya Misri kabla ya kuanza msimu huu akiwa kama Mfalme baada ya kuiongoza Yanga kutwaa mataji mawili tofauti ambayo ni Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la CRDB.

Hata hivyo upepo unaonekana kumuendea vibaya kocha huyo ndani ya Ismaily kutokana na mwenendo usioridhisha ambao imekuwa nayo katika Ligi Kuu ya Misri tangu msimu huu ulipoanza.

Timu hiyo katika mechi tano ilizocheza msimu huu, inashika nafasi ya 17 katika msimamo wa Ligi Kuu ya Misri ikiwa imevuna pointi nne tu ambazo zimetokana na ushindi katika mechi moja na sare moja.

Mchezo pekee ambao Ismaily iliibuka na ushindi ni dhidi ya El Geish ilipopata ushindi wa bao 1-0 Agosti 24 mwaka huu na sare pekee ya timu hiyo ni dhidi ya Petrojet, Agosti 9 ambapo ilipata matokeo ya sare tasa.

Mbali na hizo, Ismaily imepoteza mechi tatu dhidi ya timu za Pyramids, Al Ittihad na Mehalla El Ghazl.

Mchezo dhidi ya Pyramids ilifungwa bao 1-0 kama ilivyokuwa dhidi ya Al Ittihad na dhidi ya Mehalla El Ghazl, ikapoteza kwa mabao 3-0.

Kabla hajajiunga na Ismaily, Hamdi alifanikiwa kutwaa tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara tatu ndani ya miezi minne kutokana na kuiongoza Yanga kufanya vyema.

Tuzo ya kwanza alishinda mwezi februari na ya pili aliipata ya mwezi Aprili na mara ya mwisho akaitwaa ya mwezi Juni.

Hamdi aliiongoza Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la CRDB katika msimu uliopita ambao pia aliiongoza kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Msimamo wa Ligi Kuu ya Misri kwa sasa unaongoza na Al Masry yenye pointi 11 ikifuatiwa na Zamalek na Modern ambazo kila moja ina pointi 10 huku Petrojet ikiwa nafasi ya nne na pointi zake tisa.

Pyramids FC iko katika nafasi ya tano ikiwa na pointi nane na mabingwa wa kihistoria wa ligi hiyo, Al Ahly wakiwa nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi tano.