Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Morocco yaifungashia virago Zambia CHAN 2024

Muktasari:

  • Morocco sasa imesogea hadi nafasi ya pili kwenye kundi A ikifikisha pointi sita.

Timu ya Taifa ya Morocco imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Zambia ambayo rasmi imeaga mashindano ya CHAN baada ya kucheza mechi tatu bila kupata ushindi.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya imeshuhudiwa Simba wa milima ya Atlas wakipata ushindi huo kupitia mabao yaliyofungwa na Mohamed Hrimat ambaye amefunga bao la kwanza dakika ya 45  na kuipeleka mapumziko Morocco ikiwa kifua mbele.

Kipindi cha pili, Zambia ilirudi kivingine, safari hii ilionekana kutafuta bao la kusawazisha ambapo ilijaribu kufanya mashambulizi kadhaa kwenye lango la Morocco mpaka ilipokuja kuandika bao dakika ya 65 ambalo lilifungwa na kiungo, Happy Nsiku.

Hata hivyo, bao hilo lilikataliwa na Teknolojia ya VAR baada ya kugundulika kuwa mfungaji alifanya madhambi kabla ya kuingiza mpira wavuni.

Dakika mbili baadaye Oussama Lamlioui aliifungia Morocco bao la pili akimalizia kwa kichwa mpira wa krosi.

Zambia iliendelea kufanya mashambulizi na safari hii Andrew Phiri alifanikiwa kufunga bao la kwanza na kuleta matumaini kwa vijana hao wa Chipolopolo.

Hata hivyo, matumaini ya kusawazisha yalizimwa na Sabir Bougrine ambaye aliifungia Morocco bao la tatu katika dakika za nyongeza na kukamilisha ushindi wa mabao 3-1.

Morocco sasa imesogea hadi nafasi ya pili kwenye Kundi A ikifikisha pointi sita na kuishusha Angola yenye pointi nne ambayo baadae itakuwa dimbani katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya DR Congo.

Hadi sasa Morocco imecheza mechi tatu huku ikisubiri kucheza mechi ya mwisho Agosti 17 dhidi ya DR Congo.

Wenyeji wa mashindano hayo Kenya ndiyo wanaongoza kundi kwa pointi saba baada ya kushinda mechi mbili na kupata sare mechi moja. Harambee Stars licha ya kuongoza kundi hilo bado inasubiri mechi ya mwisho dhidi ya Zambia ambayo itaamua kufuzu kwao hatua ya robo fainali.