Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Morrison amfuata Nabi Morocco

Dar es Salaam. Aliyekuwa winga wa Yanga, Bernard Morrison yupo nchini Morocco na taarifa za uhakika ni kwamba anafukuzia dili la kuwatumikia mabingwa wa nchi hiyo FAR Rabat.

FAR Rabat ambayo sasa inafundishwa na kocha wa zamani wa Yanga Nasreddine Nabi inapiga hesabu za kumchukua Morrison wakiwa kwenye msako wa kusaka winga kulingana na mahitaji ya kocha huyo mpya ambaye hatahivyo awali akiwa nae Jangwani alikuwa hamkubali kiviile.

Taarifa za ndani kutoka kwa mtu wa karibu na Morisson zimeliambia Mwananchi kuwa mchezaji huyo raia wa Ghana yupo nchini humo na kama mambo yataenda sawa atasaini miaka miwili.

Mbali na majaribio hayo pia winga huyo huenda akapewa mkataba mgumu kutokana na Nabi tayari ana faili lake la jinsi alivyoishi naye ndani ya Yanga.

FAR Rabat inasaka mawinga wawili wa kulia na kushoto katika kuboresha kikosi hicho ambacho msimu ujao kitashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.