Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpanzu alivyoizamisha Singida BS

Winga wa Simba, Elie Mpanzu, (watatu mbele kutoka kulia), akishangilia pamoja na wachezaji wenzake baada ya kuifungia timu yake bao la ushindi katika mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Singida Black Stars. Picha na Simba

Singida. Bao la dakika ya 84 la Ellie Mpanzu limeipa Simba ushindi wa mabao 2-1 ugenini kwenye Uwanja wa Airtel, Singida leo, Jumatano, Machi 11, 2026 dhidi ya Singida Black Stars.

Mpanzu ambaye aliingia uwanjani katika dakika ya 79 kuchukua nafasi ya Jospin Loemba, alifunga bao hilo kwa shuti la mguu wa kushoto akiunganisha pasi ya Clatous Chama.

Simba ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao katika mchezo huo kupitia kwa Anicet Oura katika dakika ya saba.

Aura alifunga bao hilo kwa mguu wa kulia akimaliza pasi ya kichwa ya Allasane Kante aliyetumia vyema kosa la kipa wa Singida Black Stars kuupangua vibaya mpira wa kona iliyochongwa na Clatous Chama.

Baada ya kuingia kwa bao hilo, Singida Black Stars ilianza kufunguka na kupishana na Simba na juhudi zake zilizaa matunda katika dakika ya 37 ilipopata bao la kusawazisha lililopachikwa na Ndumumwe Mossi.

Mossi alifunga bao hilo kwa kichwa akimalia krosi iliyopigwa na Lamin Jarju. Hadi timu hizo zinamaliza kipindi cha kwanza, matokeo yalikuwa ni sare ya bao 1-1.

Dakika nane baada ya filimbi ya kuanza kipindi cha pili, Simba ilifanya mabadiliko ya kumtoa Allasane Kante na kumuingiza Baraka Mwangosi.

Timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu huku kila moja ikipoteza nafasi kadhaa ambazo zilitengenezwa hadi dakika ya 84, Simba ilipopata bao la ushindi kupitia kwa Mpanzu.

Matokeo hayo yameifanya Simba kufikisha pointi 27 ambazo ziliisogeza hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.