Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msuva akabidhiwa Mreno Algeria

Dar es Salaam. JS Kabylie ambayo anaichezea Simon Msuva imemtambulisha Mreno, Rui Almeida kurithi mikoba ya aliyekuwa kocha wa muda, Mohamed Lacet. 

Kocha huyo mpya wa Msuva anauwezo wa kuongea lugha sita ambazo ni Kireno, Kiitaliano, Kihispania, Kiarabu, Kiingereza na Kifaransa, hivyo akiwa na chama hilo atakuwa na uwanja mpana wa kufanya mawasiliano na wachezaji wake.

Mara baada ya utambulisho wake, Almeida alisema yupo tayari kushirikiana na viongozi, wachezaji na mashabiki kuhakikisha wanarejesha ufalme wa klabu hiyo ambayo iliwahi kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili.

“Ninafuraha kupata nafasi ya kuwa sehemu ya klabu hii kubwa na ya kipekee. Tunatakiwa kufanya kazi hatua kwa hatua ili kufanikisha kile ambacho kila mmoja wetu anatamani kukiona, siku zote nimekuwa kocha mwenye kupenda soka zuri na ushindi,” alisema.

Almeida amewahi kufanya kazi na Panathinaikos, Sporting, Braga na Zamalek kama msaidizi wa Jesualdo Ferreira kabla ya kuwa kocha mkuu wa Red Star ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza Ufaransa ‘Ligue 2’.

Mei 30, 2018, Almeida alitangazwa kuwa kocha wa Troyes katika Ligue 2, kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kuchana na Bastia. Aliiongoza timu hiyo hadi nafasi ya tatu, pointi moja nje ya kupanda daraja, katika msimu wake pekee na kisha akahusishwa na klabu ya England, West Bromwich Albion. 

Baada ya kuondoka Troyes alizifundisha Caen, Gil Vicente na msimu uliopita alikuwa na Niort kabla ya kufanya uamuzi wa kuja Afrika kujiunga na klabu ya JS Kabylie, ambayo Mtanzania huyo anachezea.