Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namba zinavyoinyima England ubingwa Euro

Muktasari:

  • England imepangwa kukutana na Switzerland baada ya kumaliza hatua ya makundi ikiwa kinara wa kundi C ikikusanya pointi tano katika mechi tatu.

Berlin, Ujerumani. Takwimu za hatua ya makundi ya mashindano ya mataifa ya Ulaya (2024) zinazoendelea Ujerumani zinawalazimisha nyota wa England kubadilika na kufanya kazi ya ziada katika mechi zinazofuata za hatua za mtoano ili kutimiza ndoto ya kutwaa kwa mara ya kwanza ubingwa wa mashindano hayo.

Timu hiyo inayonolewa na kocha Gareth Southgate imeonekana kuzidiwa kwa takwimu mbalimbali za kitimu na hata zile za mchezaji mmojammoja kutokana na kile kilichofanyika katika hatua ya makundi ya mashindano hayo ambayo ilifikia tamati juzi Jumanne huku kesho hatua ya 16 bora ikifungua mtoano.

Katika hatua ya 16 bora, England imepangwa kukutana na Switzerland baada ya kumaliza hatua ya makundi ikiwa kinara wa kundi C ikikusanya pointi tano katika mechi tatu na iwapo itapata ushindi katika mchezo huo ulio mbele yake, itakutana na mshindi wa mechi baina ya Uholanzi na Uturuki kwenye nusu fainali.

Hadi inamaliza hatua ya makundi, England imeshindwa kuingia katika tano bora ya timu ambazo zimefunga idadi kubwa ya mabao ambapo imejikuta ikishika nafasi ya tisa katika chati ya timu zilizofumania nyavu mara nyingi baada ya kufunga mabao manne tu katika mechi tatu za kundi lake.

Ujerumani ndio kinara katika chati ya ufungaji mabao hadi sasa ikiwa nayo 10, ikifuatiwa na Hispania yenye mabao tisa na timu Uholanzi, Switzerland na Uturuki zinafuata kwa kufunga mabao saba kila moja.

Katika chati ya timu zilizoshambulia mara nyingi, England imeshindwa kuingia hata katika 10 bora ambapo ipo nafasi ya 12 ikiwa imefanya mashambulizi 44.

Timu tano vinara katika kufanya mashambulizi na idadi ya mashambulizi kwenye mabano ni Hispania (84), Ureno (74), Ujerumani (71), Ufaransa (69) na Uholanzi (63).

England inashika nafasi ya tano katika orodha ya timu zilizopiga pasi sahihi ambapo yenyewe ina wastani wa asilimia 89.5 sawa na Ureno iliyo nafasi ya nne, kinara ikiwa ni Ujerumani yenye asilimia 92.3, Hispania ina asilimia 91 na Ufaransa iko nafasi ya tatu ikiwa na wastani wa asilimia 90.5 ya pasi sahihi.

Timu hiyo hadi sasa imepata kona 18 tu ambazo ni nusu ya idadi ya kona ambazo Ureno inayoongoza chati ya timu zilizopiga kona nyingi kwenye hatua ya makundi inazo na inashika nafasi ya 12 kwenye chati ya vinara wa koba ambapo nafasi ya pili inashikwa na Ujerumani iliyopiga kona 31, Hispania (kona 29) huku Uholanzi na Denmark kila moja ikipiga kona 27.

Katika chati ya timu zilizoruhusu nyavu zao kutikiswa mara chache, England iko nafasi ya tano ikiwa imefungwa mabao mawili sawa na Serbia na Ujerumani huku Hispania na Ufaransa zikiwa vinara ambapo kila moja imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara moja.

Kwa upande wa takwimu za mchezaji mmojammoja, hadi sasa hakuna mchezaji yeyote wa England ambaye amefanikiwa kuongoza chati kwenye vipengele muhimu vya mashindano hayo.

Chati ya ufungaji bora inaongozwa na Georges Mikautadze wa Georgia mwenye mabao matatu huku Jude Bellingham wa England akiwa nafasi ya tano na mabao yake mawili.

Hakuna mchezaji yeyote wa England katika 10 bora ya nyota waliopiga pasi nyingi za mwisho kwenye hatua ya makundi ambapo hadi sasa kinara ni Michel Aebischer wa Switzerland aliye na pasi za mwisho mbili.