Namungo, Al Hilal hakuna mbabe

namungo pic
namungo pic

Muktasari:

  • Namungo ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 37 lililofungwa na winga wake, Shiza Kichuya kabla ya Al Hilal kusawazisha katika dakika ya 90 kupitia kwa nyota wake, Yasser Awad.

MABINGWA wa  Sudan, Al Hilal wamelazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo katika mchezo wake wa kwanza wa kirafiki hapa nchini uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Namungo ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 37 lililofungwa na winga wake, Shiza Kichuya kabla ya Al Hilal kusawazisha katika dakika ya 90 kupitia kwa nyota wake, Yasser Awad.

Al Hilal iliwasili Jumatatu kwa mualiko maalumu wa Simba ikiwa ni sehemu ya makubalino ya mkataba uliopo baina ya timu hizo mbili inayojiwinda na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika na Mamelodi Sundowns.

Miamba hii ya Sudan inakumbukwa zaidi baada ya kuiondosha Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifunga kwa jumla ya mabao 2-1 katika hatua ya pili na kuifanya kuangukia kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Baada ya mchezo huu, Al Hilal itacheza na Azam Januari 31 kwenye Uwanja wa Azam Complex kisha itacheza na Simba Februari 5 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na kuhitimisha ziara yake ya siku 10 hapa nchini.