Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NCBA Junior Golf kuwa endelevu

Muktasari:

  • Amesema watoto 98 kutoka kwenye klabu tofauti za gofu nchini wameshiriki wakishindana katika madaraja tofauti.

Dar es Salaam. Mashindano ya gofu kwa vijana (NCBA Golf Junior Series) sasa yatakuwa endelevu yakifanyika katika mikoa tofauti nchini, imeelezwa.

Hayo yamebainishwa wakati wa kufungwa kwa mashindano hayo msimu huu yaliyofanyika kwa siku mbili kwenye viwanja vya gofu Lugalo yakilenga kuibua vipaji vya mchezo huo nchini.

Watoto 98 kutoka klabu za Dar es Salaam Gymkhana, Zanzibar Gymkhana, Morogoro Gymkhana, Kili Golf, TPC Moshi na wenyeji Lugalo walichuana katika madaraja mbalimbali msimu huu.

Akizungumza wakati wa kufungwa kwa mashindano, Mkurugenzi na ofisa mtendaji mkuu (CEO) wa benki ya NCBA Tanzania, Claver Serumaga amesema wataendelea kusapoti mashindano hayo.

Amesema, mashindano ya kuanzia mwakani, yatafanyika  shule zitakapokuwa zikifungwa.

"Kamati ya maandalizi iseme mapema ni wapi yatafanyika, yakifanyika Morogoro au kwingineko tutawasafirisha watoto kwenda kuchuana na kuendelea kuibua na kuendeleva vipaji hivi ambavyo ni hazina kwenye mchezo wa gofu," amesema Serumaga.

Akizungumzia mashindano hayo, Mwenyekiti wa klabu ya gofu Lugalo, Brigedia Jenerali, Michael Luwongo (mstaafu) amesema yalifanyika katika madaraja mbalimbali kulingana na umri wa watoto hao.

"Haya mashindano yametokana na wazo la klabu ya Lugalo la kufundisha watoto wa umri kati ya miaka 4-18 ili kuendeleza vipaji vyao,  tukaanzisha mashindano haya ambayo mdhamini mkuu ni NCBA," amesema.

Amesema watoto 98 kutoka kwenye klabu tofauti za gofu nchini wameshiriki wakishindana katika madaraja tofauti.

"Kwa kuwa ni wadogo, wengine hawawezi kucheza viwanja 18, hivyo kulikuwa kuna madaraja, wapo waliocheza viwanja vitatu, tisa na viwanja 18 ambao hawa wa viwanja 18 wamechuana kwenye daraja A,B na C

Amesema baadhi ya waliochuana kwenye viwanja 18, wapo waliopata handcep na wanatambulika kwenye mchezo huo kimataifa.

"Hii ni ishara kwamba kama taifa tayari tuna hazina ya wachezaji wa gofu  wa umri mdogo, vijana hawa baadhi yao sasa wapo wenye sifa kushindana mashindano ya kimataifa kwa kuwa wamepata handcep ambazo zinawatambulisha katika levo hiyo, " amesema Luwongo na kuongeza.

"Hata katika scores zao walizopiga wapo wenye sifa ya kucheza timu ya taifa, hii ni hazina ya taifa katika mchezo wa gofu na habari njema ni kwamba mdhamini wetu (NCBA) ametuahidi kuendelea kusapoti mashindano haya, ili vijana wetu wazidi kushindana na kuboresha vipaji vyao," amesema.

Katika mashindano hayo, mabingwa walikabidhiwa medali na baadhi ya vifaa vya gofu kutoka kwa wadhamini huku washiriki wote wakipewa zawadi mbalimbali.

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania, Boniface Tamba aliwapongeza klabu ya gofu Lugalo kwa kuwa na wazo hilo ambalo linakwenda kuboresha timu ya taifa ya mchezo huo.

"Nimeambiwa haya ni mashindano makubwa kwa vijana hapa nchini, hii ni hatua kubwa," amesema Tamba huku akiwataka viongozi wa gofu nchini kufika Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ili kuona ni namna gani ya kulichakata ombi lao la kupata unafuu kwenye vifaa vya gofu ambavyo kwa sasa gharama yake ipo juu