Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndoto ya shujaa Cape Verde yatimia, mama atua Marekani

Kile kilichotajwa kuwa kikwazo kikubwa cha kiutawala na kifedha sasa kimegeuka kuwa muujiza wa kihistoria baada ya mama mzazi wa kipa shujaa wa Cape Verde, Vozinha kufanikiwa kutua nchini Marekani.

Tukio hili la kusisimua linajiri siku chache tu baada ya kipa huyo mwenye umri wa miaka 40 kumwaga machozi mbele ya kamera kufuatia sare ya 0-0 dhidi ya Hispania, akieleza kusikitishwa na kutokuwepo kwa mama yake mzazi uwanjani kwa sababu ya changamoto za viza na gharama za tiketi.

Habari hiyo iliyogusa mioyo ya mamilioni ya mashabiki mtandaoni ilisababisha kampeni kubwa ya kidiplomasia na kibinadamu, na leo hii mama huyo amewasili salama jijini New York nchini Marekani tayari kuelekea jukwaani kumshuhudia mwanawe akiliwakilisha taifa hilo la visiwani.


Machozi ya simanzi, furaha

Baada ya kumalizika kwa mchezo wa kwanza wa Kundi H ambapo Vozinha aliokoa mipira ya hatari saba  dhidi ya mabingwa wa Ulaya, kipa huyo alifunguka kuwa na upweke wa kutokuwa na wazazi na walezi wake na kumliza.

 Alitaja kuwa babu na bibi yake waliofanya kazi kubwa ya kumlea walishafariki dunia, na pigo kubwa zaidi lilikuwa mama yake mzazi kukwama nyumbani Cape Verde kwa kukosa viza na fedha za kusafiria.

Kilio kile hakikuwa cha huzuni pekee, bali kilikuwa ni wito wa msaada uliosikika na mamlaka mbalimbali za kimataifa pamoja na mashirika ya ndege yaliyojitolea kufanikisha safari hiyo ya haraka.


Nguvu ya mitandao ya kijamii

Pia, kasi ya kusambaa kwa mahojiano ya Vozinha ilivunja mipaka ya soka.

Ndani ya saa 24, video yake ilitazamwa na mamia ya mamilioni ya watu, ikivutia hisia za mastaa wakubwa wa soka duniani na mashirika ya kutoa misaada.

Kufuatia msukumo huo wa umma, ubalozi na Idara ya Uhamiaji ya Marekani ilifanya mchakato wa dharura wa kupitisha viza ya mama huyo ndani ya muda mfupi (fast-tracked visa approval).

Wafadhili na mashabiki waligharamia tiketi za ndege za daraja la kwanza (First Class) na malazi ya kifahari ili kuhakikisha anafika New York bila usumbufu wowote.


Zaidi ya soka

Ujio wa mama huyo nchini Marekani unatafsiriwa kama ushindi mkubwa wa kiutu unaovuka mipaka ya mchezo wa soka.

Ni uthibitisho kuwa nyuma ya kila mwanamichezo anayefanya vizuri, kuna hadithi ya dhabihu kubwa, mapambano ya wazazi, na sala za chini kwa chini zisizochoka.

Vozinha amewaonyesha vijana wengi duniani umuhimu wa kuwaheshimu na kuwakumbuka wazazi hata pale mtu anapofikia kilele cha mafanikio makubwa ya kidunia.

Mwanamke huyo sasa anajiandaa kuelekea uwanjani kuungana na maelfu ya mashabiki wa Cape Verde, tayari kumpa nguvu mwanawe ambaye amekuwa mmoja wa makipa wanaozungumziwa zaidi kwenye mashindano haya ya dunia ya mwaka huu 2026.

Imeandikwa na Noor Shija kwa msaada wa mtandao.