Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pedro awatangazia vita Al Ahly, wenyewe wajibu mapigo

Muktasari:

  • Yanga itakuwa mwenyeji wa Ahly kwenye mchezo wa nne wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, utakaopigwa kesho kuanzia saa 10:00 jioni.

Zanzibar. Yanga itakuwa na mchezo mgumu kesho kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar dhidi ya Al Ahly huku kocha wao Pedro Goncalves akitangaza vita kwamba wapo tayari hata leo kucheza na mabingwa hao wa kihistoria Afrika.

Yanga itakuwa mwenyeji wa Ahly kwenye mchezo wa nne wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, utakaopigwa kesho kuanzia saa 10:00 jioni.

Akizungumza kwenye mkutano wa maandalizi ya mchezo huo, Pedro amesema kama hata ingekuwa leo inapigwa mechi hiyo, kikosi chake kipo tayari kukutana na Ahly.

Pedro amesema timu yake imefanya maandalizi uwanjani na hata nje ya Uwanja ambapo wamejipanga kutafuta pointi tatu nyingine mbele ya Ahly.

"Tumekuwa na mazoezi ya uwanjani lakini pia kule hotelini tumekuwa tunafanya vikao na wachezaji wote na mchezaji mmoja mmoja, kama mechi ingekuwa inatakiwa kuchezwa Leo tungekuwa tayari.

"Tunakwenda kucheza na timu bora ambayo inahistoria kubwa ya mafanikio, tunajua kwamba tulipoteza kwao. Tunataka kucheza kwa nidhamu mchezo wa kesho kwa kila idara ili tushinde,” alisema Pedro.

Wakati Pedro akisema hivyo mwenzake wa Ahly, Jesse Thorup amesema wanataka kushinda mechi hiyo lakini wanatambua kwamba watakutana na upinzani mkubwa.

Thorup amesema Yanga ina timu nzuri yenye wachezaji wenye ufundi lakini kikosi chake kitaingia na hesabu za kucheza kwa falsafa zao kuweza kushinda.

"Hatutakuwa na mchezo rahisi, tunajua tunaongoza kundi lakini tunataka kukaa eneo bora zaidi kwenda hatua inayofuata.

"Tunajua kwamba wapinzani wetu Wana timu nzuri, Wana wachezaji wenye ufundi na ubora mkubwa kitu muhimu hapa ni sisi kucheza soka letu ili tushinde,” amesema Thorup.

Thorup pia amethibitisha klabu hiyo kumuacha Misri kiungo tegemezi, Emam Ashour kwa sababu za kinidhamu.

Thorup raia wa Denmark amesema kiungo huyo atapewa adhabu Kali kwa makosa ambayo ameyafanya ambapo timu hiyo itaendelea na mechi zake bila ya uwepo wake.

"Nathibitisha kwamba hatutakuwa na Ashour, amefanya makosa ya kinidhamu na atapewa adhabu kali, amebaki nyumbani.

"Nilikuwa nasema tangu nimefika hapa,hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu, staa peke tuliyenaye hapa ni Al Ahly, tunahitaji kuwa na nidhamu.

"Tumeshajiandaa kucheza mechi zinazofuata bila yeye(Ashour) tunataka Kila mmoja atambue kwamba ukifanya makosa utachukuliwa hatua,” amesema Throup