Pilato Simba , Yanga huyu hapa

MWAMUZI Ahmed Arajiga wa Manyara anatarajia kutoa hukumu katika mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho (ASFC), itakayowakutanisha Simba na Yanga.

Vigogo hao wanatarajia kushuka katika uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma Julai 25 katika fainali inayompa bingwa nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa kwa upande wa Shirikisho.

Simba na Yanga tayari wao washakata tiketi ya ushiriki wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kumaliza katika nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa msimamo wa Ligi Kuu hivyo nafasi hiyo watachukua Azam na Biashara United.

Mbali na mwamuzi huyo wa kati wengine ni Frednand Chacha kutoka Mwanza pamoja na Mohamed Mkono kutoka Tanga.

Mwamuzi wa akiba atakuwa Elly Sasii kutokea Dar es Salaam.

Nassoro Hamduni kutoka Kigoma atakuwa mfatiliaji na msimamizi wa waamuzi wakati msimaizi wa masuala ya utimamu wa miili atakuwa, Shabani Shata kutokea Kigoma.

Msimamizi wa masuala ya kinidhamu atakuwa, Jaqcqueline Kamwamu kutokea Dar, msimamizi wa masuala ya matangazo ya kibiashara, Fredrick Masolwa (Dar).

Mechi dokta, Suphian Juma wa Dar, Ofisa habari, Clifford Ndimbo, msimamizi wa usalama, Filemon Makungu (Kigoma).

Wengine msaidizi wa kusimamia mechi, Tunda Shaban (Dar) na Harieth Gilla (Dar).

Msimamizi wa mechi atakuwa, Baraka Kizuguto kutokea Dar es Salaam, na msimamizi wa kati ni Omary Gindi kutokea Dar es Salaam.