Rayvany amfuata Harmonize

Muktasari:

Rayvanny ambaye anatesa na wimbo wa ‘Kiuno’ leo Jumanne, Februari 9, 2021, kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram ameweka picha zinazoonyesha zitakapokuwepo ofisi za lebo hiyo na jina huku akiipa jina la ‘Next level Music’.

Rayvany amfuata Harmonize. ndivyo unavyoweza kusema baada ya msanii kutoka lebo ya WCB, Raymond Mwakyusa maarufu Rayvanny kuja na lebo yake.

Rayvanny ambaye anatesa na wimbo wa ‘Kiuno’ leo Jumanne, Februari 9, 2021, kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram ameweka picha zinazoonyesha zitakapokuwepo ofisi za lebo hiyo na jina huku akiipa jina la ‘Next level Music’.

Ujio wa lebo hiyo kwa Rayvany, utafanya kuwa msanii wa pili kuwa na lebo, huku akitanguliwa na Harmonize ambaye alijiengua mapema mwaka juzi na kuanzisha lebo yake ya Konde Gang ambayo mpaka sasa ina wasanii watano.

Pia tayari msanii huyo hivi karibuni aliachaia albamu yake inayokwenda kwa jina la ‘Sound from Africa’ ambayo inafanya vizuri katika mitndao mbalimbali ya kuuzia kazi za muziki.

Swali ni je baada ya kuja na lebo hiyo, je yeye atabaki WCB au naye ataondoka mazima ili kuwapa wasanii wengine nafasi?