Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rekodi tisa kichapo cha Yanga

Muktasari:

  • Mabao ya Tabora United katika mechi hiyo yalifungwa na Ofen Chikola aliyepachika mawili na lingine moja likiwekwa kimiani na Nelson Munganga na bao pekee la Yanga lilipachikwa na Clement Mzize.

Dar es Salaam. Ushindi wa mabao 3-1 ambao Tabora United iliupata dhidi ya Yanga jana kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam umefanya kumbukumbu kadhaa kuwekwa na baadhi ya rekodi kuandikwa au kutoendelezwa kwa timu mojawapo kati ya hizo.

Mabao ya Tabora United katika mechi hiyo yalifungwa na Ofen Chikola aliyepachika mawili na lingine moja likiwekwa kimiani na Nelson Munganga na bao pekee la Yanga lilipachikwa na Clement Mzize.

1-Kwa kupata ushindi huo, Tabora United imepata ushindi kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu dhidi ya Yanga na pia kuzuia bingwa huyo mtetezi asiendeleze rekodi ya ubabe dhidi yao kwani kabla ya hapo iliwafunga mechi zote mbili walizokuwa wamewahi kukutana.

3-Matokeo hayo yameifanya Tabora United kuandika rekodi ya kupata ushindi katika mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu kwa mara ya kwanza kwani tangu ilipopanda daraja msimu uliopita haikuwahi kufanya hivyo.

1759-Hii ni mara ya kwanza kwa Yanga kuruhusu nyavu zake zitikiswe mara tatu katika mechi moja ya Ligi Kuu baada ya siku 1759 (miaka minne na miezi tisa na siku 24), kupita tangu ilipofanya hivyo.

3-Kabla ya Tabora United, timu ya mwisho kuifunga Yanga mabao matatu ilikuwa ni Kagera Sugar iliyoibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa ligi uliochezwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Januari 15, 2020.

2-Huu ni msimu wa kwanza baada ya misimu minne mfululizo kupita kwa Yanga kupoteza mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu tangu ilipokutana na vipigo viwili mfululizo katika msimu wa 2019/2020 ambapo ilifungwa mabao 3-0 na Kagera Sugar kisha ikapoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Azam FC.

6-Baada ya misimu mitatu mfululizo ya ubabe, Yanga kwa mara ya kwanza imeangusha pointi sita katika mechi 10 za mwanzo tangu ilipofanya hivyo kwa mara ya mwisho msimu wa 2020/2021.

10-Katika mechi 10 za mwanzo kwenye msimu wa 2020/2021, Yanga iliangusha pointi sita kwa kutoka sare mechi tatu kati ya 10 za mwanzo ambapo ilimaliza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba na kisha ikapata matokeo kama hayo dhidi ya Tanzania Prisons na ilitoka suluhu na Gwambina huku ikipata ushindi katika mechi nyingine saba.

3-Kuruhusu mabao matatu katika mchezo mmoja wa ligi kwa kipa Djigui Diarra kunafanya iwe mara ya kwanza kwake kufungwa idadi hiyo ya mabao katika mchezo mmoja wa ligi kwani tangu alipojiunga na Yanga mwaka 2021, hajawahi kufungwa mabao matatu katika mchezo mmoja wa ligi kuu.

1-Mambo yameonekana kuwa tofauti kwa Yanga katika Uwanja wa Azam Complex kwani tangu imeanza kuutumia, haijawahi kufungwa mabao matatu katika mchezo mmoja katika mashindano tofauti iliyocheza hapo, huu ni wa kwanza.


Kauli ya Gamondi

Akizungumzia matokeo ya juzi, kocha Miguel Gamondi alisema kuwa anawajibika kwa hicho kilichotokea ingawa kuwakosa wachezaji wake muhimu anaamini kumechangia kuifanya timu yake ipoteze mechi hiyo.

"Siwezi kutoa kisingizio chochote, timu ikishinda kila mtu anafurahi ila timu ikifungwa ni wajibu wa kocha, kufungwa mimi ndio nawajibika.

"Tumecheza mechi sita (6) kwenye siku ishirini na moja (21) pamoja na kusafiri na nililalamikia hili kabla ya mechi na Black Stars, ni mbaya kwetu ila tunahitaji kuwa na uvumilivu," alisema Gamondi.

Yanga sasa inajiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal utakaopigwa Novemba 28 jijini Dar es Salaam.