Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo hatihati kukosa mechi Kombe la Dunia 2026

Muktasari:

  • Kadi nyekundu ya moja kwa moja inaweza kumfanya akose mechi ya ufunguzi wa Kombe la Dunia mwaka ujao ikiwa Ureno itafuzu.

Mshambuliaji nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo, ana hatari ya kukosekana kwenye mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Dunia baada ya kupewa kadi nyekundu ya kwanza kabisa katika timu ya taifa kwenye mchezo dhidi ya Ireland, uliopigwa jana usiku.

Ronaldo alitolewa nje dakika ya 60 baada ya kumgonga kwa bega, beki wa Ireland, Dara O’Shea kwenye mchezo ambao Ureno ilijikuta ikipoteza 2-0 jijini Dublin matokeo ambayo hayakutarajiwa.

Nyota huyo anayekipiga kwenye Klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia alionekana kukosa utulivu kutokana na kiwango hafifu ilichokionesha Ureno. Kabla ya tukio lake, alionekana kumkejeli beki wa Ireland, Nathan Collins, kana kwamba “analialia”.

VAR yabadili kadi ya njano kuwa nyekundu

Awali mwamuzi alimpa Ronaldo kadi ya njano, lakini baada ya VAR kutazama tukio, uamuzi ukabadilishwa na kuwa kadi nyekundu ya moja kwa moja. O’Shea alianguka huku akishika mgongo wake baada ya mkono wa Ronaldo kumfikia wakati wa kugombania krosi iliyompita.

Ronaldo aliondoka uwanjani kwa hasira, akiwapigia mashabiki makofi kabla ya kuelekea kwenye mlango wa vyumba vya kubadilishia nguo. Pia alionekana kulalamikia benchi la Ireland, akitamka “hongereni” kwa dharau, hadi alipozuiwa na Ricardo Carvalho.

Athari kwa mechi za Ureno

Kwa kadi hiyo, Ronaldo atakosa mchezo wa mwisho wa kufuzu dhidi ya Armenia utakaochezwa Jumapili. Lakini pigo kubwa zaidi ni kwamba kadi nyekundu ya moja kwa moja inaweza kumfanya akose mechi ya ufunguzi wa Kombe la Dunia mwaka ujao ikiwa Ureno itafuzu. Kwa mujibu wa FIFA, kadi za njano hazivuki mashindano, lakini nyekundu huvuka.

Kocha Roberto Martinez alimtetea nahodha wake akisema hakukuwa na vurugu:

“Alikuwa anasukuma tu kujitoa kwenye mtego, lakini bahati mbaya VAR ikaonyesha kama jambo kubwa kuliko lilivyokuwa, Aliahidi kuwa mtoto mzuri kabla ya mechi, Cha kushangaza, saa chache kabla ya mchezo, Ronaldo alihadithia wanahabari kuwa angetulia:

“Najua mashabiki wa hapa wanapenda timu yao. Natarajia wasinipigie kelele sana. Nataka kuwa mvulana mzuri kesho,” alisema.

Ireland yatinga hatua muhimu

Ushindi wa Ireland wa 2-0 unaipa matumaini makubwa ya kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 2002. Wako pointi moja tu nyuma ya Hungary ambayo watachezanayo mchezo Jumapili.

Troy Parrott ndiye shujaa wa usiku huo baada ya kufunga mabao yote mawili.

“Huu ndiyo usiku bora zaidi katika maisha yangu,” alisema akiwa amefurahi mno.

Alifunga la kwanza dakika ya 16 kwa kichwa, na kuongeza la pili kwa shuti kali lililompita Ruben Dias na kipa Diogo Costa.

Kocha Heimir Hallgrimsson alisema wachezaji wake walionesha nidhamu na umoja mkubwa:

“Ronaldo alipoteza utulivu, alijua hakutakiwa kufanya kile alichofanya,” alisema akitoa maoni yake kuhusu tukio la kadi nyekundu.