Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu za Dembele kuikosa Arsenal leo

Muktasari:

  • Dembele amekuwa kwenye kiwango cha juu kwenye timu hiyo msimu huu kwenye michezo yote aliyoshiriki.

London, England. Staa wa PSG Ousmane Dembele, ataukosa mchezo wa leo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal baada ya kukorofishana na kocha wa timu hiyo Luis Enrique.

PSG inatarajiwa kuvaana na Arsenal kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ukiwa ni mchezo wa pili wa michuano hiyo msimu huu baada ya Arsenal kucheza dhidi ya Atalanta kwenye mchezo wa awali na kutoka suluhu, huku PSG ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Girona.

Dembele amekuwa kwenye kiwango cha juu kwenye timu hiyo msimu huu kwenye michezo yote aliyoshiriki.

Staa huyo mwenye miaka 27, alijibishana na kocha wake kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Ufaransa dhidi ya Rennes baada ya kutolewa uwanjani kabla mchezo huo haujamalizika.

Dembele amekuwa akitajwa kuwa ndiye mbadala sahihi wa Kylian Mbappe ambaye tangu ameondoka na kujiunga na Real Madrid Juni mwaka huu, amefanikiwa kufunga mabao manne kwenye michezo sita ya timu hiyo ya Ufaransa.

Mbappe msimu wake wa mwisho na PSG alifanikiwa kufunga mabao 44 kwenye michezo 48 akiwa ndiye alikuwa mchezaji mahiri zaidi kwenye timu hiyo kwa kipindi chote alichokaa hapo.

Akizungumzia kwanini Dembele hayupo kwenye msafara wa PSG, Enrique alisema: "Kama mtu hawezi kuwa na heshima na kufuata maagizo wakati wa maandalizi ya timu ina maana kuwa hayupo tayari kucheza.

"Mechi yetu ni muhimu sana na nataka kuona kila mchezaji anatakiwa tayari, hivyo nimemuacha Dembele kwa sababu hizo, nataka kuona kila mchezaji anaonyesha kiwango kizuri kwenye timu hii.

"Ninaungwa mkono na rais wa klabu pamoja na Mkurugenzi wa Ufundi. Nipo hapa kwa ajili ya kutengeneza timu bora Dembele akiwemo, kwa uhalisia mimi sina shida binafsi naye," alisema kocha huyo wa zamani wa Barcelona.

Hata hivyo, baada ya kukosekana kwa staa huyo, sasa majukumu ya timu kwenye eneo la ushambuliaji yanabaki kwa Bradley Barcola, ambaye amefanikiwa kuonyesha uwezo mzuri kwenye michezo iliyopita, huyu ni mchezaji mahiri akiwa amefunga mabao sita kwenye michezo sita ya Ligue 1 msimu huu, mawili akiwa amefunga dhidi ya Rennes.

Staa huyo mwenye miaka 22 anatajwa kuwa mmoja kati ya mastaa wakubwa wajao kwenye Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1.


Mechi nyingine za Uefa leo

Dortmund vs Cetic

Slovan vs Man City

RB Sazburgvs Brest

Barcelona vs Young Boys

VfB Stuttgart vs Sparta Praha

Inter vs Crvena