Simba wapimwa corona, kuanza mazoezi mchana

Thursday March 04 2021
COVID PIC
By Thobias Sebastian

BAADA ya kuwasili Addis Ababa, Ethiopia kisha kupumzika na kuendelea na safari kwenda Khartoum, Sudan msafara wa wachezaji, viongozi na benchi la Simba ulifika saa 9:00 usiku na kuelekea moja kwa moja hotelini.

Simba imefikia katika hoteli yenye hadhi ya nyota tano inayoitwa Salam ambayo ipo katikati ya mji wa Khartoum hapa Sudan.

Msafara huo wa Simba baada ya kufika hotelini hapo wachezaji, viongozi  na benchi la ufundi walikwenda moja kwa moja katika vyumba vyao ili kupumzika.

Saa 5 asubuhi wachezaji walienda kwenye vipimo vya covid 19 baada ya kupata kifungua kinywa kwenye hoteli waliyofikia.

Baada ya kumaliza vipimo vya covid 19, wachezaji walitakiwa kwenda kupumzika ili kusuburi ratiba ya chakula cha mchana saa 6:30.

Mara baada ya kumaliza kula chakula cha mchana watapumzika kwa saa moja na saa 8:30 watakuwa katika uwanja wa mazoezi wakifanya mazoezi ya kwanza hapa Sudan.

Advertisement
Advertisement