Simba yajitoa Kagame, wachezaji wapewa mapumziko

Simba imetangaza kujitoa kwenye mshindano ya Kagame yanatotarajiwa kufanyika mapema Agosti jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa timu Simba, Abbas Ally amesema hawashiriki Kagame ili kutoa nafasi kwa wachezaji kupumzika.
“Tumetoka kwenye Ligi ya Mabingwa halafu tukaunganisha kucheza Ligi Kuu na sasa tumemalizia Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kwa kishindo kwa kutwaa ubingwa dhidi ya watani wetu.
“Wachezaji wanahitaji mapumziko hata kama ni kwa muda mfupi lakini itawasaidia kuweka miili sawa. Baada ya siku 10 za mapumziko watarejea kambini,” amesema Abbas.
Abbas amesema wamekuwa na misimu minne mizuri ikiwemo kuchukua  ubingwa wa ligi  mara nne mfululizo pia kutwaa ubingwa wa ASFC mara mbili mfululizo.
“ Tumeweka historia ya kutwaa mataji na kumfunga mtani na kuchukua ubingwa mbele yake. Kwenye ligi walituvimbia  ila kwenye ASFC tumechukua ubingwa kilaini ,” amesema Abbas