Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yasaka Mkurugenzi wa Ufundi, vigezo vyaanikwa

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji akiwa anaongoza moja ya kikao cha bodi hiyo. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Mkurugenzi wa Ufundi katika soka ana majukumu kuandaa na kusimamia mipango ya muda mrefu ya kiufundi, usajili wa wachezaji, usimamizi wa makocha, soka la vijana na kuwa daraja baina ya uongozi na benchi la ufundi.

Dar es Salaam. Simba imetangaza nafasi mbili za ajila ndani ya Klabu hiyo huku mojawapo ikiwa ni ya Mkurugenzi wa Ufundi ambayo ni kwa mara ya kwanza imeanza kuwepo ndani ya klabu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Simba leo Jumamosi, Januari 31, 2026, Mkurugenzi huyo wa ufundi wa Simba atakuwa na majukumu ya kufuatilia mipango ya muda mrefu, ksuimamia usajili na uhamisho, kufanya tathmini ya benchi la ufundi na kusimamia.

Hii ni mara ya kwanza kwa Simba kuwa na mkurugenzi wa ufundi, nafasi ambayo ni daraja baina ya uongozi wa timu na benchi lanufundi.

Taarifa ya Simba imeeleza kwamba muombaji anapaswa kuwa na leseni ya ukocha ya daraja A CAF na kinyume cha hapo basi ni awe na leseni daraja A ya Umoja wa Vyama vya Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA).

Sifa nyingine ni awe na shahada ya kwanza au stashahada ya Sayansi ya Michezo au utawala na pia awe na ufahamu wa mifumo ya kisoka.

Mbali na nafasi hiyo, Simba pia imetangaza nafasi ya Mkurugenzi wa Wanachama ambayo katika miaka ya hivi karibuni ilikuwa inashikiliwa na Mzee Hamisi Kisiwa).

Kwa mujibu wa taarifa ya Simba, Mkurugenzi huyo wa Wanachama wa Simba anapaswa awe angalau ana uzoefu wa miaka mitatu wa nafasi hiyo au inayofanana nayo na awe na shahada ya kwanza masoko, utawala wa kibiashara.

Taarifa ya Simba imeeleza kuwa Mkurugenzi huyo wa wanachama atatakiwa kufanya mambo manne ya msingi ambayo ni usajili wa wanachama, kuwakutanisha pamoja wanachama na kufanya nao mawasiliano, kufanya tathmini ya data na mkakati, kuongeza idadi ya wanachama.