Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yasaka mrithi wa Chama, Yanga kushusha mchana nyavu 

Muktasari:

  • Muda uliobakia ni mchache tangu dirisha la usajili Tanzania Bara lifungwe huku kila timu zikitaka kulala bila deni ambapo Simba inasaka mrithi wa Chama na Sima ikitarajiwa kushusha mtambo wa mabao.

Dar es Salaam. Zikiwa zimesalia saa chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa, wababe wa Msimbazi, Simba wamekamilisha dili la mshambuliaji Pa Omar Jobe, raia ya Gambia. 

Tayari mshambuliaji huyo ameshasaini mkataba wa miaka miwili na kutambulishwa rasmi, lakini mabosi wa Simba wako bize kusaka kiungo mshambuliaji wa viwango vya juu kabla dirisha la usajili kufungwa rasmi.

Mwananchi linafahamu kuwa mezani kwa mabosi wa Simba kuna majina ya wachezaji watatu ambayo yanachambuliwa kabla ya kupatikana staa moja atakayepewa mkataba Msimbazi.

Kocha Abdelhak Benchikha amewataka viongozi wa klabu yake kuhakikisha wanasajili kiungo mshambuliaji kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye eneo hilo.

Itakumbukwa kuwa Simba kwa sasa wako kwenye mgogoro na kiungo mshambuliaji wake, Clatous Chama ambaye kwa sasa amesimamishwa kwa utovu wa nidhamu.

Habari za ndani zinaeleza kwamba, huenda msimu ujao kikosi cha Simba kikwa bila Chama, ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

“Tuko kwenye mikakati ya kupata kiungo mshambuliaji kwa ajili ya kuongeza, tuna uhakika tutafanikisha hili kabla ya muda wa dirisha kufungwa,” kilisema chanzo chetu ndani ya klabu hiyo.

Licha ya Chama kuwa kwenye mgogoro na klabu yake, kwa sasa yupo na kikosi cha timu ya Taifa Zambia nchini Ivory Coast katika Fainali za Mataifa Afrika.


Yanga nako hakujalala

Wakati Simba wakiendelea kuimarisha kikosi chake, mashabiki wa Yanga wanasubiri ahadi ya viongozi kumshusha mshambuliaji mpya, ambaye kwa sasa yupo safarini kutua nchini muda wowote.

Mshambuliaji huyo anakuja kuchukua nafasi ya Hafiz Konkoni, ambaye ameshindwa kuonyesha makali yake kwenye kikosi cha Jangwani. Taarifa za uhakika zinasema kwamba, kabla ya kufikia saa 6:00 usiku kila kitu kitakuwa hadharani.

Imeelezwa kuwa kwa sasa Yanga inakamilisha mazungumzo ya mwisho na mshambuliaji huyo kupitia mabosi wao Rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said ambaye yuko nje ya nchi.

Huo ndio usajili pekee ambao unasubiriwa na kocha wa Yanga, Miguel Gamondi ambaye ujio wa mshambuliaji utasaidia kuongeza ufanisi kwenye kikosi chake.