Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sura mbili kufutwa msamaha kodi vifaa vya michezo

Muktasari:

  • Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amepongeza hatua hiyo akibainisha kwamba vifaa vya michezo ni muhimu kwa maendeleo ya mpira wa miguu na michezo yote.

Dar es Salaam. Wakati Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2025/26 ikianisha kufutwa kwa msamaha wa kodi kwenye ununuaji na uingizaji wa vifaa vya michezo 'gaming supply', wadau wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya hatua hiyo.

Jana Juni 12, 2025 akisoma Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/26 bungeni mjini Dodoma,  Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema kufuta msamaha wa kodi kwenye ongezeko la thamani unaotolewa kwenye ununuaji na uagizaji wa vifaa vya michezo kunalenga kuleta usawa katika utozaji wa kodi kwa michezo mingine.

Alitolea mfano mpira wa miguu akibainisha ipo katika wigo wa kodi ya ongezeko la thamani na kubainisha hatua hiyo inalenga kuongeza mapato ya serikali kwa kiasi cha Shilingi bilioni 322.


Wadau wakosoa, wapongeza

Akizungumzia kufutwa kwa msamaha huo wa kodi, aliyewahi kuwa Katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah amesema katika vifaa vya michezo Serikali ilipaswa kuangalia kwa jicho la tatu ni vifaa gani vinahitaji msamaha huo na vipi vifutiwe.

"Mwanzo nilijua ni vifaa kama viatu na jezi ambavyo ni muhimu sana, hata hivyo kwa kuwa kuna michezo ya profesheno (kulipwa) na amature (ridhaa), ningetamani serikali ingeliangalia hilo.

"Ingezingatia msamaha kwenye vifaa vya michezo vya watoto na vile vya mafunzo, hii ingesaidia tasnia ya michezo kwani watoto hawachezi kibiashara, unapoweka kodi kwenye vifaa vyao maana yake unawanyima fursa ya kutumia vifaa sahihi hivyo kuwarudisha nyuma," amesema.

Akitolea mfano wa nyasi bandia, Osiah amesema Serikali ilipoweka msamaha kwenye nyasi bandia viwanja vingi vilibuka hadi vya watu binafsi na kuboreshwa.

"Hadi uswahilini, kulijengwa viwanja vya nyasi bandia," amesema Osiah.

Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi amesema bajeti haikufafanua ni vifaa vipi ambavyo vimefutwa msamaha wa kodi.

"Bajeti imezungumzia moja kwa moja vifaa vya michezo, wengi walifikiri ni kama jezi, viatu, suti za michezo na vifaa vingine ambvyo havikuwa na msamaha wa kodi.

"Msamaha wa kodi kuna wakati walisamehe kwenye nyasi bandia, ambazo zinawagusa zaidi watu wa soko, riadha inakimbiliwa kwenye tartan track(kapeti ya kukimbilia), vipi kuhusu michezo kama netiboli? voleyball na mingine ambayo viwanja vyao si vya nyasi bandia? alihoji Bayi.

Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amepongeza hatua hiyo akibainisha kwamba vifaa vya michezo ni muhimu kwa maendeleo ya mpira wa miguu na michezo yote.

"Binafsi naona kufutwa kwa msamaha wa kodi kwenye vifaa vya michezo 'gaming supply' ni uamuzi sahihi," alisema Rage kwa kifupi.

Celestine Mwesigwa, Katibu mkuu wa zamani wa Yanga amezungumzia changamoto ya kodi katika vifaa vya michezo na kueleza huwa inaiathiri sekta hiyo kwa kiasi kikubwa.

"Sijui Serikali imeangalia nini kufuta msahama wa kodi kwenye vifaa hivyo, lakini kama mdu wa michezo jambo hili linsikitisha, ingawa hatufahamu huenda wamefuta huko lakini kuna sehemu watalet unafuu," amesema.

Amesema ni kazi kuingiza vifaa vya michezo, akigusia ambavyo vinahusu soka kama nyasi bandia, mipira, jezi na vifaa vingine ambavyo gharama ni kubwa.

"Inaleta unafuu huku ingesaidia sana, mfano kuna misaada huwa inatoka Fifa (Shirikisho la Soka la Kimataifa), CAF (Shirikisho la Soka Afrika) sasa mtu akupe msaada kisha akulipie na kodi ni ngumu," amesema Mwesigwa.