Taifa bado kumepoa

Saturday September 25 2021
taifapic
By Olipa Assa
By Charity James

Dar es Salaam. Kinachoendelea uwanja wa Benjamin Mkapa, kunakosubiriwa kupigwa mechi ya Ngao ya Jamii, kati ya Simba na Yanga kuna maeneo mapya yamezibwa tofauti na ilivyozoeleka mwanzo.

Timu hizo zikiwa na majukumu yake katika uwanja huo, maeneo yanayokuwa yanazibwa mwanzoni na mwisho wa barabara ya kwenda Keko ndiyo yanakubwa yanafungwa.

Kizuizi kipya walichokiongeza leo ni katikati ya uwanja wa Benjamin Mkapa, hivyo barabara hiyo imekuwa na utulivu wa hali ya juu, tofauti na nyomi ya mashabiki inavyojaa siku zote.

Kizuizi hicho kimewasaidia polisi wa kulinda usalama kwa muda huu, kutokuwa na purukushani za kuwaelekeza mashabiki maeneo wanayotakiwa kupitia.

Mbali na hilo, bado hadi muda huu hakujachangamka kama ilivyozoeleka timu hizo zikichezwa mapema mashabiki wanakuwa wamekiwasha.

Ukiachana na hilo, hakuna foleni ya mashabiki kuingia ndani wala ya kukataa tiketi.

Advertisement
Advertisement