Tanzania yapanda viwango FIFA

Tanzania yapanda viwango FIFA

Muktasari:

  • Tanzania imepanda kwa nafasi mbili katika viwango vya ubora wa soka kwa mwezi Oktoba vilivyowekwa hadharani leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA).

Tanzania imepanda kwa nafasi mbili katika viwango vya ubora wa soka kwa mwezi Oktoba vilivyowekwa hadharani leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA).

Kutoka nafasi ya 132 iliyokuwepo katika viwango vya mwezi Septemba, Tanzania imesogea hadi nafasi ya 130 katika orodha ya viwango vipya ambayo FIFA wameitoa leo, Alhamisi, Oktoba 21.

Ushindi wa bao 1-0 ambao Tanzania iliupata dhidi ya Benin katika mechi ya hatua ya makundi ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia kwa upande wa bara la Afrika, Oktoba 10 umeonekana kuchangia kwa kiasi kikubwa Tanzania kupanda kwa nafasi hizo mbili.

Tanzania imepanda hadi nafasi hiyo ya 132 baada ya kufikisha jumla ya pointi 1123.84 kutoka zile 1115.37 ilizokuwa nazo mwezi uliopita.

Wakati Tanzania ikipanda, majirani zake wa Afrika Mashariki, Kenya wameporomoka kwa nafasi mbili kutoka ile ya 102 waliyokuwepo awali hadi nafasi ya 104 ambayo wameangukia kwa viwango vya mwezi Oktoba.

Rwanda imeanguka kwa nafasi tano kutoka ile ya 128 hadi nafasi ya 133 wakati Burundi imebaki katika nafasi ya 141 iliyokuwepo hapo awali.

Uganda imeendelea kuwa kinara kwa upande wa ukanda wa Afrika Mashariki baada ya kupanda kwa nafasi nne kutoka ile ya 86 hadi nafasi ya 82 mtawalia