Try Again: Mchakato wa mabadiliko umebaki kwa wanachama

Try Again: Mchakato wa mabadiliko umebaki kwa wanachama

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi klabu ya Simba, Salim Abdallah 'Try Again' amesema mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo kwa sasa umebaki kwa wanachama.

Try Again amebainisha hayo kwenye mkutano mkuu wa klabu ya hiyo hii leo na kueleza kwamba ili wafunge mjadala huo na klabu kuanza kujiendesha kwa mtindo wa hisa, wameiongezea nguvu kamati ya mabadiliko.

"Murtaza Mangungu, Mwenyekiti wa klabu ya Simba na Hussein Kitta, mjumbe wa bodi wameongezwa kwenye kamati ambayo mwenyekiti anabaki yule yule Aziz Kifile na katibu, Mulamu Nghambi na maadam CEO, Barbara Gonzalez.

Amesema kwa upande wa mwekezaji tayari mchakato umekamilika, na Mohammed Dewji aliweka Sh20 bilioni miezi kadhaa iliyopita.

"Katika pesa hizo za mwekezaji, Sh200 millioni tumepata kwa mwezi kama 'enterest', hivyo kilichopo kwa sasa ni kwa wanachama wetu kuhakikiwa na kufanya uhamisho wa mali za klabu.