UDSM yaichapa SUA tamasha la michezo Moro

Wachezaji wa soka kati ya timu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na wenzao wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kabla ya mchezo ambapo katika mchezo huo UDSM imeshinda 2-0.Picha na Juma Mtanda.

Muktasari:

Katika michezo hiyo Sua imeambulia vipigo katika mchezo wa soka, netiboli, basketiboli huku wageni hao wakipoteza katika mchezo mmoja wa kuvuta kamba wanaume.

Morogoro. Timu ya soka ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) imepeleka kilio kwa mashabiki na uongozi wa timu ya soka ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Morogoro baada ya kuibuka na ushindi mnono wa bao 2-0 katika mchezo mkali wakati wa tamasha la michezo lililofanyika uwanja wa chuo kikuu hicho mkoani hapa.

Akizungumza na Mwanaspoti katika tamasha la michezo mkoani hapa, Mlinda mlango wa timu ya soka ya UDSM, Faraji Ghaibu alisema kuwa kwa upande wao wamefurahi kupata ushindi mbele ya SUA kwa kuwachapa bao 2-0.

Faraji alisema kuwa timu ya SUA imekuwa sumbufu kwao baada ya kuwatoa nishai katika michezo ya Shimuta yaliyofanyika mwaka jana mkoani Tanga kwa bao 2-0.

“Jamaa huwa wanatusumbua sana na mwaka jana katika mashindano ya Shimuta kule Tanga mwaka jana SUA walitoandoa katika robo fainali kwa kutuchapa bao 2-0 na sisi leo kama tumelipa kisasi kwa kuwatandika bao 2-0 japo haina umuhimu sana lakini tuna furaha kwani tumelipa kisasi tena katika uwanja wao wa nyumbani.’alisema Faraji.

Mabao ya washindi hao yalipachikwa wavuni na washambuliaji Taliki Kasanje na Dk Armstrong Matogwa.

Naibu makamu wa mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (Utawala), Profesa Bonaventure Rutinwa alisema kuwa ushindi wao katika tamashala hilo umetokana na uongozi kutoa sapoti na kufanya maandalizi ya kutosha kwa wachezaji wao kabla ya kwenda Morogoro ktika michezo mbalimbali.

Profesa Rutinwa alisema kuwa chuo kikuu chao kinaipa kipaumbele michezo na haikushangaza kupata ushindi dhidi ya wapinzani wetu kwani katika michezo minne iliyoshuka dimbani wameweza kupata ushindi mnono.

“Unaweza kuona katika michezo minne tofauti katika tamasha hili katika soka tumweza kuibuka na ushindiwa bao 2-0 huku netibali vijana wangu wakishinda kwa bao 44-24 na baskabali nako tukiwaliza kwa vikapu 57-26 na wao SUA wakishinda mchezo mmoja tu wa kuvuta kamba waume 2-0.”alisema Profesa Rutinwa.


Kwa upande wa Naibu makamu wa mkuu wa chuo taalumu katika chuo kikuu cha Sokine cha kilimo (SUA) Morogoro, Profesa Maulidi Mwatawala alisema kuwa tamasha hilo lina lengo la kudumisha undugu kati ya SUA na chuo kikuu cha Dar es Salaam.

 “Tumecheza michezo minne ya soka, netiboli, basketiboli, kuvuta kama wanaume na michezo hii ina imarisha undugu wetu kati ya SUA na UDSM na kabla ya SUA kupata hadhi ya chuo kikuu SUA ilikuwa tawi la chuo kikuu na mwaka 1985 ndio itangazwa kuwa chuo kikuu rasmi.”alisema Propesa Mwatawala.