Ulimwengu atinga Stars kivingine

Muktasari:

Ulimwengu ameonekana katika mazoezi hayo akiwa na muonekano mpya wa kutoa staili yake ya nywele ‘Kiduku’ na kunyoa kawaida lakini alisema kuwa ameamua kubadilisha tu mtindo wa nywele tofauti na alivyozoeleka machoni mwa watu.

Mshambuliaji AFC Esikilistuna ya Sweden, Thomas Ulimwengu ni miongoni mwa wachezaji wa Taifa Stars waliofanya mazoezi leo kwenye Viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youths  Park Center.

JKanayecheza  ni amezungumzia maisha ya nchini Sweden kuwa ni sehemu yenye watu wenye utulivu na umoja  na wachezaji pia wanapendana kuona kila mmoja akifanya vizuri katika klabu yao.

Ulimwengu ameonekana katika mazoezi hayo akiwa na muonekano mpya wa kutoa staili yake ya nywele ‘Kiduku’ na kunyoa kawaida lakini alisema kuwa ameamua kubadilisha tu mtindo wa nywele tofauti na alivyozoeleka machoni mwa watu.

Stars itaondoka kesho Jumanne saa nne asubuhi kwenda kambini Misri kwa ajili ya maandalizi ya Mashidano ya CHAN katika mechi za mchujo zianzotarajiwa kuanza mwezi June.

Wachezaji waliofanya mazoezi ni  Aishi Manula, Beno Kakolanya, Said Mohamed ‘Nduda’, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Nurdin Chona, Abdurahman Mussa, Simon Msuva, Hassan Kessy, Salum Aboubacary ‘Sure Boy’, Mbaraka Yusuph, Salim Mbonde, Said Ndemla, Shiza Kichuya, Said Ndemla, Abdi Banda na Mohammed