Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ushindi wa Arsenal waibeba Ligi Kuu England Ulaya

Mshambuliaji wa Arsenal, Kai Havertz wakati akifunga bao la ushindi katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Sporting CP. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Arsenal haijapoteza mechi zote 11 za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu ikishinda michezo 10 na kutoka sare mechi moja.

Ushindi wa bao 1-0 ambao Arsenal imeupata ugenini dhidi ya Sporting Lisbon jana usiku, umekuwa na neema kwa Ligi Kuu England (EPL).

Matokeo hayo yameihakikishia EPL kuwa na timu tano katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, ikiwa ni mara ya pili mfululizo.

Hiyo imetokana na Ligi ya England kukusanya idadi kubwa ya pointi kutokana na ufanisi wa klabu zake katika mashindano ya Ulaya.

Hata ikitokea timu za England zikashindwa kufika hatua za juu za mashindano hayo, Ligi hiyo imejihakikishia kumaliza katika nafasi mbili bora za juu za ligi zilizofanya vizuri katika mashindano ya klabu Ulaya ambazo kila moja itawakilishwa na timu tano.

England inaweza kuwakilishwa na timu sita msimu ujao ikiwa klabu yake moja itafanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Europa League ambalo kwa sasa timu za Nottingham Forest na Aston Villa ziko robo fainali.

Msimu uliopita, EPL iliwakilishwa na timu sita ambazo ni Arsenal, Chelsea, Man City, Liverpool, Newcastle United na Tottenham Hotspur.

Ligi ya Hispania ‘La Liga’ inaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kuwa ligi ya pili ambayo itapata fursa ya kuwa  na klabu tano katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Katika mchezo wa jana, bao pekee la Arsenal lilifungwa katika dakika za majeruhi na Kai Havertz akimalizia pasi ya Gabriel Martinelli.

Mchezo mwingine wa Ligi ya Mabingwa Ulaya jana ulimalizika kwa kichapo cha mabao 2-1 ambacho Real Madrid ilikipata kutoka kwa Bayern Munich.