Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal kukipiga na Sporting CP robo fainali Ulaya

Muktasari:

  • Arsenal sasa itakutana na Sporting CP katika hatua ya robo fainali, baada ya timu hiyo ya Ureno kupindua matokeo ya mabao 3-0 ilipofungwa ugenini na kushinda 5-0 nyumbani dhidi ya Bodo/Glimt.

London, England. Mabao mawili kutoka kwa Eberechi Eze na Declan Rice, yameisaidia Arsenal kupata ushindi wa 2-0 nyumbani dhidi ya Bayer Leverkusen na kufuzu hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Arsenal sasa itakutana na Sporting CP katika hatua ya robo fainali, baada ya timu hiyo ya Ureno kupindua meza ikitoka nyuma kwa mabao 3-0 ilipofungwa ugenini na kushinda 5-0 nyumbani dhidi ya Bodo/Glimt.

Katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Emirates usiku wa Jumanne Machi 17, 2026 timu zote ziliingia zikiwa sare baada ya penalti ya dakika za mwisho ya Kai Havertz wiki iliyopita kuifanya mechi ya kwanza kumalizika kwa sare ya 1-1.

Arsenal ilikaribia kufunga mara mbili kupitia Gabriel Magalhães kwa mipira ya kona, lakini kipa wa Leverkusen, Janis Blaswich alifanya kazi nzuri na kuzuia nyavu zake zisitikiswe.

Hata hivyo, hakuweza kuzuia bao la kwanza, ambapo Eze aliutuliza mpira nje kidogo ya eneo la hatari na kupiga shuti kali lililoingia wavuni likiwa bao lake la kwanza kwenye mashindano hayo.

Arsenal iliendelea na kasi hiyo kipindi cha pili, na Rice akahitimisha ushindi huo baada ya kupachika kwa utulivu bao la pili.

Baada ya kuhakikisha ushindi, kocha Mikel Arteta alipata nafasi ya kuwapumzisha baadhi ya wachezaji wake muhimu kabla ya Arsenal kukutana na Manchester City kwenye fainali ya Kombe la Carabao itakayochezwa katika Uwanja wa Wembley, Jumapili hii Machi 22, 2026.