Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PSG yaitupa nje Chelsea ikiisubili Liverpool au Galatasaray

Muktasari:

  • Khvicha Kvaratskhelia alifungua ukurasa wa mabao mapema dakika ya sita, kabla ya Bradley Barcola kuongeza bao la pili dakika ya 14 kwa shuti lao la pili tu kuelekea golini.

London, England. Chelsea imepata kichapo kizito katika mechi mbili za mtoano Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikipoteza kwa jumla ya mabao 8-2 baada ya usiku wa Jumanne Machi 17, 2026 kufungwa 3-0 dhidi ya mabingwa wa Ulaya, Paris Saint-Germain kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Khvicha Kvaratskhelia alifungua ukurasa wa mabao mapema dakika ya sita, kabla ya Bradley Barcola kuongeza bao la pili dakika ya 14 kwa shuti lao la pili tu kuelekea golini.

Matokeo hayo yalizima kabisa ushindani wa mechi hiyo, huku mchezaji wa akiba Senny Mayulu akiongeza machungu kwa Chelsea katika mchezo huu wa hatua ya 16 bora akifunga bao la tatu dakika ya 62.

Mashabiki wa nyumbani walisikika wakiimba jina la mmiliki wa zamani Roman Abramovich, licha ya Ligi Kuu England kutoa faini ya rekodi ya pauni 10.75m kufuatia zaidi ya pauni 47m zilizolipwa kwa mawakala bila kutangazwa. Pia kulikuwa na nyimbo za kulalamikia uongozi wa sasa uliokuwepo jukwaa la wageni maalum.

Bao la kwanza lilitokana na uzembe wa beki Mamadou Sarr, uliompa nafasi Kvaratskhelia kuwahi mpira na kufunga kwa shuti la chini kwa mguu wa kushoto.

Chelsea ilijaribu kujibu mashambulizi kupitia Cole Palmer, Enzo Fernandez, Pedro Neto na Trevoh Chalobah kabla ya PSG kufunga bao la pili.

Baada ya Moises Caicedo kupoteza mpira katikati ya uwanja, PSG ilifanya shambulizi la kushtukiza na Barcola akaonyesha ufundi wa hali ya juu kwa kuudhibiti mpira kwa mguu wake dhaifu kabla ya kupiga shuti la nusu-voli lililojaa wavuni.

Chelsea iliendelea kushambulia na kupata nafasi kupitia Joao Pedro, Palmer na Jorrel Hato, lakini pia iliendelea kutoa nafasi nyingi kwa wapinzani wao kupitia Kvaratskhelia na Barcola.

Wachezaji wa Chelsea walizomewa na mashabiki wao wakati wa mapumziko, hali iliyomlazimu kocha mkuu, Liam Rosenior kufanya mabadiliko kwa kumtoa Sarr na kumuingiza chipukizi Josh Acheampong.

Baadhi ya wachezaji wa PSG wakishangilia baada ya kusonga katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuifunga Chelsea jumla ya mabao 8-2. Picha na Mtandao

Kipindi cha pili, Joao Pedro alikaribia kufunga dakika ya 56, lakini muda mfupi baadaye Rosenior alionekana kukata tamaa kwa kuwatoa wachezaji muhimu Palmer, Fernandez na Joao Pedro.

Liam Delap alipata nafasi ya karibu lakini shuti lake liliokolewa, kabla ya Mayulu, mwenye umri wa miaka 19, kufunga bao la tatu kwa shuti la kuvutia lililotoka nje kidogo ya eneo la hatari, na kuifanya PSG ishinde kwa jumla ya mabao 8-2. Kumbuka mechi ya kwanza ugenini Chelsea ilifungwa 5-2.

Usiku huo mbaya kwa Chelsea uliendelea pale beki Chalobah alipoumia na kutolewa nje kwa machela, na kuwaacha wenyeji wakicheza na wachezaji 10 katika dakika za mwisho.

PSG sasa itakutana na mshindi kati ya Liverpool dhidi ya Galatasaray, ambapo klabu ya Uturuki inaongoza kwa bao 1-0 kabla ya mchezo wa marudiano utakaochezwa Anfield, usiku wa Jumatano Machi 18, 2026.