Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sporting ilivyopindua meza kibabe, Bodo ikishindwa kushika bomba

Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha Sporting CP, wakati wakishangilia baada ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Kichapo hicho kimehitimisha safari ya kihistoria ya Bodo/Glimt katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu 2025-2026 baada ya Sporting kuonyesha moyo wa ajabu wa kupambana, wakifuta pengo la mabao 3-0 kutoka mechi ya kwanza ugenini na hatimaye kushinda kwa jumla ya 5-3 baada ya muda wa nyongeza, na kutinga robo fainali kwa mara ya kwanza.

Pale katika Uwanja wa José Alvalade jijini Lisbon nchini Ureno mbele ya mashabiki 49,155 waliofika uwanjani hapo, wameshuhudia Bodo/Glimt ikishindwa kushikilia bomba kwa Sporting CP na kukubali kichapo cha mabao 5-0.

Kichapo hicho kimehitimisha safari ya kihistoria ya Bodo/Glimt katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu 2025-2026 baada ya Sporting kupindua meza na kufuta pengo la mabao 3-0 kutoka mechi ya kwanza ugenini na hatimaye kushinda kwa jumla ya 5-3 baada ya muda wa nyongeza, na kutinga robo fainali kwa mara ya kwanza.

Klabu hiyo ya Norway ilikuwa miongoni mwa simulizi kubwa za msimu huu, ikiwa timu ya kwanza kutoka nchini humo kufika hatua ya mtoanohuku ikishiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza baada ya kuwatoa washindi wa pili wa msimu uliopita, Inter Milan, katika hatua ya mchujo.

Mshambuliaji wa Sporting CP, Luis Suarez wakati akishangilia moja ya bao alilofunga katika ushindi wa 5-0 ilioupata Sporting CP dhidi ya Bodo/Glimt katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Picha na Mtandao

Waliendeleza ndoto yao kwa kuifunga Sporting mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza, lakini wamekuja kukumbana na kibarua kigumu zaidi nchini Ureno.

Ndivyo ilivyokuwa, huku lango la Bodo likishambuliwa mara kwa mara katika kipindi cha kwanza, kabla ya Sporting kupata bao la kuongoza dakika ya 34 kupitia kichwa cha Goncalo Inacio.

Wageni walitumia muda mwingi wa dakika 45 za kwanza kujilinda, lakini walikaribia kufunga walipopiga mwamba wa lango kupitia kichwa cha Odin Bjortuft kilichotokana na kona yao ya kwanza.

Sporting waliendeleza presha na kuhakikisha kunakuwa na dakika 30 za mwisho zenye presha kubwa walipoongeza bao la pili dakika ya 61, Luis Suarez alipotoa pasi na Pedro Goncalves kuachia shuti kali lililojaa nyavuni.

Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha Sporting CP, wakati wakishangilia moja ya bao katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Bodo/Glimt katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Picha na Mtandao

Kuanzia hapo mashambulizi yalikuwa mfululizo kutoka kwa Sporting, na wakasawazisha jumla ya mabao (aggregate) pale Suarez alipofunga kwa penalti dakika ya 78 baada ya Fredrik Bjorkan kuonekana kuunawa mpira kufuatia mapitio ya VAR.

Sporting waliendelea kusaka bao la ushindi ndani ya muda wa kawaida, huku Nuno Santos akigonga mwamba wa lango kwa shuti la mbali.

Hata hivyo, baada ya muda wa nyongeza dakika 30 kutokana na 90 kumalizika kwa Sporting kuwa mbele kwa mabao 3-0 na kufanya matokeo ya jumla kuwa sare ya 3-3, Sporting walipata bao muhimu mapema dakika ya 92 kupitia Maxi Araujo, akiwapa uongozi wa jumla, kabla ya Rafael Nel kufunga bao la mwisho dakika ya120+1 lililokamilisha ushindi huo wa kusisimua na kuhitimisha safari ya ndoto ya Bodo/Glimt.