Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usiyoyajua kuhusu bondia Feriche Mashauri

Ni Mzaliwa wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma lakini makazi yake kwa sehemu kubwa ya shughuli za kimaisha zipo ndani ya Jiji la Dar es Salaam ambalo linasimamiwa na mkuu wa mkoa Albert Chalamila.

Huyu ni mwanadada halafu pia ni mama wa familia bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Feriche Mashauri lakini wengi katika mchezo wa ngumi huwa wanamfananisha na Scot Adkins staa wa filamu ya Boyka Undisputed kutokana na kujaliwa nguvu na maarifa ya kupigana.

Bondia huyo ambaye kwa mujibu wa rekodi yake amepanda ulingoni katika mapambano 20 ambayo sawa na raundi 101 ikiwa kila raundi moja inamjumuisho wa dakika mbili za kupigana ambayo ni tofauti na wanaume wanaopigana kwa dakika tatu katika kila raundi moja.

Mashauri amefanikiwa kushinda mapambano 11 kati ya hayo ameshinda kwa Knockout mara tatu peke yake lakini amepigwa mara nane kati ya hizo tatu ni kwa Knockout na ametoka sare moja huku akicheza kwenye uzani wa light.

Mashauri amefichua kuwa sababu kubwa iliopelekea kumvutia kuingia katika mchezo wa ngumi ni kutokana na tabia yake ya kupenda kupigana tangu alipokuwa shule ingawa hakujua mapema kama itakuja kuwa ajira yake.

"Kilichonivutia kuwa bondia kwanza ni kupenda kupigana maana shule nilikuwa napigana ila sikujua kuwa ni ajira, sasa baadaye katika  ukuaji wangu ndiyo nilitambua ni kazi kama kazi zingine.

"Lakini kwa kuongezea huwezi ukapenda kitu kama hupendi ila ukweli napenda sana kupigana.

Kwa nini mabondia wa kike hawapewi kipaumbele cha kupigana mara kwa mara?

"Hatupewi kipaumbele kwa sababu ya sisi wenyewe mabondia kutokana na  kuogopana au kuchagua mtu wa kucheza naye, inatoka na kuhofia kupigwa na wewe unataka kuonekana ni bora hata kama umecheza na bondia mwepesi 'ndizi'.

"Lakini kama chama cha ngumi kinaletewa taarifa ya pambano na mwandaaji, nadhani chama  kingetutizama kwa jicho la pili kuwa hapa una mechi nane labda  basi kwakua kuna usawa weka mbili za wanawake na sita za wanaume ili kuendelea kuweka hamasa hata kwa wanaoanza au wanaotamani watoto wao waje kupigana baadaye.

"Kungekuwa na hii kanuni basi tungekuwa mbali na tungekuwa kama mabondia wakiume maana tunaona hata nchi za wenzetu mabondia wakike walivyona ushindani.

Umekutana na kitu gani cha ajabu kwenye ngumi?

"Kikubwa ambacho huwa kinatokea  kutokulipwa na si mara moja mtu anakwambia, amepata hasara, sasa wewe ukiangalia umepigana  na umeshindwa na unaona ndiyo muandaaji  huyo anategemewa kuandaa wakati mwingine, kinachotokea unaacha kudai haki yako kishingo upande ili usinyimwe tena nafasi.

"Lakini wakati mwengine muandaaji au promota anakulipa kulingana na anavyoona kiwango chako au kukuchukulia wa kawaida.


Muamko wa ngumi kwa mtoto wa kike bado umekuwa mdogo, unafikiri kwa nini?

"Nadhani kwa sababu hatupati nafasi kujitangaza kwenye biashara za watu na matangazo tofauti tofauti basi tungepata mabondia chipukizi wengi sana na pia tungefika mbali kwenye tasnia hii ya ngumi.


Wewe ni mama wa watoto wangapi?

"Nashukuru Mungu, ni mama watoto wawili.

Unawezaje kubalansi muda wa mazoezi na malez ya familia?

"Nabalansi muda wangu wa mazoezi na familia kwa sababu mazoezi nafanya asubuhi na jioni na pia kabla ya kwenda mazoezi asubuhi nakuwa nimeandaa nusu ya mahitaji ya watoto na nikirudi mchana namalizia kazi ambazo sikumaliza kisja jioni narudi mazoezini  nikirudi baada ya hapo  ni muda wa familia.


Umekuwa ukijitoa katika mambo ya kijamii lakini bado haungwi mkono?

"Nadhani kuungwa mkono ndiyo changamoto maana nilikuwa natarajia kuwa kwa kuwa mimi ndiyo bondia wa kike kufanya hili na mwitikio utakuwa mkubwa ila ni tofauti hata kwa mabondia wenzangu ukiachana na watu baki, wakati hii ni jambo la kujivunia katika tasinia yetu ya ngumi.

"Nilikuwa na malengo ya kusaidia wahitaji hospitalini na watoto yatima yaani moyo wangu unakuwaga na imani nikifanya hivyo ila tu sijakata tamaa nawaomba sana watu wajitokeze maana hujui kesho yako ikoje.


Ukimya wako umetokana na kitu gan kwenye ngumi?

"Ukimya wangu unatokana kutokupatiwa nafasi na siyo kwamba sitafutwi hapana natafutwa mara chache sana ila ofa zinazokuja ni ndogo na wengine wanakuvunja moyo kuwa sisi mabondia wa kike hatupigani kama  wanaume labda niulize wanaume kama wana ngumi mpya ambazo siyo jab, hook na uppercut.

"Huu ni mchezo hatari tunaomba vyama waweke  usawa na ndiyo maana kwa uhalisia mabondia wengi wa kike hawana mafanikio wako radhi apigane kwa 50,000, 100,000 au 500,000 au bure ili aonekane wakati umri unaenda na malengo unashindwa kutimiza kwa wakati hivyo mimi ni mzazi na pia ni tegemezi kwa familia nikisema nisubili ngumi peke yake sitoweza kufika.

Ukipewa nafasi ya kuongea na Rais Samia, utamwambia nini?

"Kwanza nitampongeza kuwa mwanamke shujaa Afrika kuwahi kutoa, Nampongeza kwa jitihada zake za kila siku kama mwanamke anayepambania majukumu yaliombele yake ila nitamwambia mama naomba aendelee kutushika mkono wanawake katika kila sekta siyo muziki na sanaa hata kwenye michezo wa ngumi tupo sawa."