Vinicius Jr afanyiwa upasuaji wa kubadili mwonekano
Muktasari:
- Nchini Uingereza gharama za upasuaji huo zinaweza kuanzia Pauni 3,000 (Sh11 nilioni) hadi zaidi ya Pauni 14,000 (Sh50 milioni), kutegemeana na aina ya matibabu yaliyofanyika.
Nyota wa Real Madrid, Vinicius Junior mwenye umri wa miaka 26 ameonekana kuwa na muonekano wa tofauti baada ya kufanyiwa upasuaji wa chini ya kidevu baada ya Brazil kuondolewa kwenye Kombe la Dunia.
Chombo cha habari cha Brazil, TMC, kimeripoti kuwa Vinicius Jr alifanyiwa upasuaji huo wa kuboresha umbo la kidevu mjini Goiania, Brazil siku chache baada ya Brazil kutolewa na Norway katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia kwa kufungwa mabao 2-1.
Katika picha aliyopiga pamoja na daktari wa ngozi, Dk Alessandro Alarcao, kidevu cha Vinicius kimeonekana kuwa tofauti na kilivyoonekana awali, kikiwa na umbo lililojitokeza zaidi.
Ingawa hakuna gharama maalumu iliyowekwa kwa utaratibu huo, nchini Uingereza gharama za upasuaji huo zinaweza kuanzia Pauni 3,000 (Sh11 milioni) hadi zaidi ya Pauni 14,000 (Sh50 milioni), kutegemeana na aina ya matibabu yaliyofanyika.
Muonekano wake mpya umeibuka wakati ambapo amethibitisha kuwa amerudiana na mpenzi wake Virginia.
Virginia alitangaza kuachana kwao kabla ya Kombe la Dunia, baada ya wawili hao kuwa kwenye uhusiano wa kuachana na kurudiana tangu walipoanza kuhusishwa kimapenzi mwaka 2025.
Hata hivyo, ilionekana wazi kuwa wamerudiana walipoonekana pamoja mwezi huu wakiwa kwenye boti ya kifahari wakifurahia muda wao pamoja.