Viwanja vitano vyapigwa 'stop' Ligi Kuu

Viwanja vitano vyapigwa 'stop' Ligi Kuu

Muktasari:

  • Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesimamisha viwanja vitano kutumika kwenye mechi za Ligi Kuu ya NBC kwa kutokidhi vigezo.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesimamisha viwanja vitano kutumika kwenye mechi za Ligi Kuu ya NBC kwa kutokidhi vigezo.

Pia Shirikisho limesema viwanja vingine vitatu vitaruhusiwa kutumika baada ya marekebisho yanayoendelea kukamilika na kupitishwa na Kamati ya Leseni za Klabu.
Viwanja vilivyosimamishwa ni Mkwawani (Tanga), Nyankumbu Girls (Geita), Ushirika (Moshi), Mabatini (Pwani), na Jamhuri (Dodoma).

Vilevile viwanja ambavyo viko kwenye marekebisho ni Majaliwa (Ruangwa, Lindi), Sokoine (Mbeya), na Kaitaba (Bukoba).
Jumla ya viwanja tisa vimepitishwa kutumika kwenye Ligi ambavyo ni Benjamin Mkapa (Dar es Salaam), Kirumba (Mwanza), Chamazi (Dar es Salaam), Highland Estate (Mbarali, Mbeya), Karatu (Arusha), Liti (Singida), Manungu (Turiani, Morogoro), Sheikh Kaluta Amri Abeid (Arusha), na Uhuru (Dar es Salaam).