Waziri Mavunde aanza kutimiza ahadi viwanja  michezo

Muktasari:

  • Waziri Mavunde ni mjumbe wa baraza la wadhamini wa Yanga na pia ni mlezi wa timu ya Dodoma Jiji.

Ujenzi wa viwanja vya michezo ya mpira wa kikapu(basketball),mpira wa pete(netball) na mpira wa wavu(volleyball) katika eneo la shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege Jijini Dodoma umeanza rasmi ukiwa ni ukifadhiliwa na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ambaye ni mbunge wa Dodoma Mjini.


                     

Mchakato huo wa ujenzi wa viwanja hivyo ni utekelezaji wa ahadi ya Mbunge Mavunde ambayo aliitoa wakati wa mahafali ya wanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo alipokuwa mgeni rasmii.

                    

Akizungumza na wanafunzi shuleni hapo  leo asubuhi alipowatembelea,Mbunge Mavunde amesema kiwanja hicho ambacho kitatumika kwa matumizi ya aina tatu ya michezo kitakuwa ni cha kisasa na kitasaidia kukuza michezo na vipaji vya wanafunzi wa Dodoma Jiji.

Pamoja na ujenzi huo,Mbunge Mavunde ameahidi kuweka taa katika uwanja huo ili uwe unatumika muda wote,kugawa seti za michezo na kununua tanki la kuhifadhi maji.

                        

Akitoa taarifa ya maendeleo ya shule,Mkuu wa Shule Sekondari Kiwanja cha Ndege Ndg. Daniel ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa madarasa na fedha Shilingi 50 milioni za umaliziaji ujenzi wa maabara na kuongeza pia kukamilika kwa ujenzi wa michezo hapo shuleni utasaidia kuimarisha afya za wanafunzi na kukuza vipaji vyao kupitia michezo.


                     

Akitoa shukrani zake,Diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Amos Mbalanga amemshukuru Mbunge Mavunde kwa ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya kuimarisha michezo na kuahidi kusimamia ujenzi wake kukamilika kwa wakati.