Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yakoub, Nangu watua rasmi Simba, wanogesha ushindani

Muktasari:

  • Nangu na Yakoub walikuwemo katika kikosi cha Taifa Stars kilichoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) 2024.

Ni rasmi kipa namba moja wa timu ya taifa 'Taifa Stars' Yakoub Suleiman na beki Wilson Nangu wataitumikia Simba msimu wa 2025/26.

Wawili hao wametambulishwa leo Septemba 3, 2025 baada ya uongozi wa Simba kukamilisha mchakato wa kuwasajilli kutoka JKT Tanzania na walikuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Simba imetoa taarifa rasmi ya kumalizana na JKT Tanzania na kuwapata nyota hao ambao wote wapo kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa na mechi mbili za kufuzu kombe la Dunia.

Usajili wa nyota hao ndani ya Simba unaongeza changamoto ya ushindani wa namba kwani tayari maeneo wanayoenda kucheza kuna wachezaji ambao tayari wamefanya vizuri.

Yakoub anaenda kupambania namba na Moussa Camara ambaye ndiye kipa chaguo la kwanza la Simba huku msimu uliopita akimaliza akiwa kinara wa kucheza idadi kubwa ya mechi bila kuruhusu bao (clean sheets) kwenye Ligi Kuu akifanya hivyo mara 19.

Kwa upande wa Nangu ambaye ameitumikia JKT Tanzania kwa msimu mmoja akitokea TMA ambayo inashiriki Championship anaenda kuongeza vita dhidi ya Abdulrazack Hamza, Rushine de Reuck na Chamou Karaboue.

Ukiondoa vita hiyo pia wachezaji hao wanaenda kuongeza upana wa kikosi kwani kwenye nafasi hizo mbili wachezaji waliokuwepo walikuwa na uhakika wa namba kikosi cha kwanza kutokana na kukosa changamoto.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally kupitia ukurasa wake wa Instagram amemkaribisha Yakoub ndani ya kikosi cha Simba kwa kumtambulisha kuwa ni Tanzania One.

Wachezaji hao wanaungana na baadhi ya wachezaji wengine ambao tayari wametambulishwa ndani ya timu hiyo ambao ni pamoja na Morice Abraham, Alassane Kante kutoka CA Bizertin, Rushine De Reuck kutoka Mamelodi Sundowns, Charles Daud Semfuko kutoka Coastal Union, Neo Maema kutoka Mamelodi Sundowns na wengine.