Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yamal: Inawezekana kupindua matokeo

Kinda wa Barcelona, Lamine Yamal, wakati akizungumza na vyombo vya habari kuelekea katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Yamal amehusika katika mabao tisa akifunga matano na kutoa pasi nne za mabao katika michezo tisa ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

Madrid, Hispania. Kinda wa Barcelona, Lamine Yamal, ametuma ujumbe kwa kocha wa Atlético Madrid, Diego Simeone ‘Cholo’ kuelekea katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Yamal, ambaye yuko kwenye kiwango bora msimu huu chini ya Meneja Hansi Flick, amesema anatamani kupata nafasi ya kukutana na beki mmoja mmoja wa Atletico ili aweze kuonyesha tofauti uwanjani.

“Najisikia vizuri sana, ninatarajia kwa hamu kubwa mchezo wa leo. Nina motisha ya hali ya juu na natumaini nitaweza kuonyesha tofauti. Tutaona kama Cholo atanipa nafasi ya kukutana uso kwa uso na beki mmoja mmoja,” amesema Yamal katika mkutano na waandishi wa habari.

Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone, alipokuwa akizungumza na Lamine Yamal katika mechi ya robo fainali ya kwanza iliyopigwa Camp Nou wiki iliyopita. Picha na Mtandao

Nyota huyo kijana amekiri kuwa mwanzoni mwa msimu kiwango chake kilikuwa kinahojiwa kutokana na majeraha lakini sasa anaona hizi ndizo nyakati sahihi za kuonyesha uwezo wake.

“Nilianza msimu huku kiwango changu kikihojiwa kutokana na majeraha, lakini napenda nyakati kama hizi kwa sababu ndipo wachezaji wa kweli hujitokeza. Ninasubiri kwa hamu mchezo wa leo,” ameongeza.

Yamal pia amewahakikishia mashabiki wa Barcelona kuwa timu itapambana hadi dakika ya mwisho kuhakikisha inapata matokeo mazuri.

Kinda wa Barcelona, Lamine Yamal. Picha na Mtandao

“Tunaahidi kwamba hata kama tutatolewa, tutakuwa tumepambana hadi mwisho. Hatutaacha kukimbia wala kushinikiza hata kwa dakika moja. Tutatoa kila kitu iwe dakika 90 au zaidi. Bado haijaisha, inawezekana kupindua matokeo na ndiyo maana tupo hapa,” amesema.

Barcelona wanakabiliwa na kibarua kigumu baada ya kupoteza mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza, hivyo wanahitaji ushindi mkubwa ili kufuzu hatua ya nusu fainali.

Hadi sasa, Yamal amehusika katika mabao tisa akifunga matano na kutoa pasi nne za mabao katika michezo tisa ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, akitarajiwa kuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika harakati za timu yake kusaka ushindi jijini Madrid.